HALI ILIVYO.
Na. John Kabambala. Utumikishwaji
wa watoto kwenye migodi ni tatizo bado kwa baadhi ya maeneo ya machimbo ya
madini nchini Tanzania. Watoto wadogo
wanashurutishwa kufanya kazi ngumu, hatari na ya kutisha katika migodi, badala
ya kupata elimu na kufurahia utoto wao. Athari za utumikishwaji huu ni mbaya
kwa maendeleo ya kimwili, kiakili, kijamii, na kiuchumi pia, Watoto hao hukabiliwa na hatari za
kiafya, kunyimwa elimu, na wanakosa fursa za kujenga ujuzi na uzoefu muhimu kwa
maisha yao ya baadaye.
Kwa kiwango
kikubwa kazi wanazo zifanyishwa watoto hawa kwenye maeneo ya migodi ni kubeba
mawe, vifusi, kuponda kokoto na hata kuchota maji yanayotumika kwenye shughuli
ndogo ndogo za migodini.
TUMEFIKAJE HAPA?
Sababu kuu
ya kuendelea kuwepo kwa utumikishwaji wa watoto kwenye migodi ni umaskini.
Familia zenye kipato cha chini zinaweza kuona utumikishwaji wa watoto kama njia
ya kuongeza kipato chao. Aidha, udhaifu wa mifumo ya elimu na uhaba wa fursa za
ajira kwa watu wazima unachangia hali hii, Serikali na jamii kwa ujumla
wanahitaji kushirikiana kikamilifu ili kukabiliana na umaskini, kuimarisha
mifumo ya elimu, na kukuza fursa za ajira ili kuvunja mzunguko wa utumikishwaji
watoto kwenye migodi.
Stefano Gwandumi siojina lake halisi nikijana mwenye umri wa
Miaka kumi na tisa mkazi wa Wilaya ya Tukuyu, katika shughuli za
uchimbaji na uchenjuaji wa madini alizianza akiwana na umri wa Miaka kumi na
tano tu, nimemkuta kwenye machimbo yajulikanayo kwa jina la merelani yaliopo
Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya hapa anazaidi ya mika mitatu kwenye machimbo haya.
Ndg. Gwandumi nilimuuliza mbinu gani huzitumia vijana kupata
kazi kwenye machimbo, wangali wanaumri mdogo? anasema lakini kwanza anataja sababu
zinazo pelekea vijana kuelekeza mawazo yao kiutafutaji kwenye machimbo, “Umasiki
wa familia yetu ndio chanzo cha kuchagua kazi za machimbo, na vijana tuliopo
huku kwenye machimbo umri wetu sio sahihi tunao usema kwa muajiri wakati wa
kutafuta au kutafutwa kwenda kufanya kazi, ili uchukuliwe lazima useme una umri
wa kuanzia miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
Anasema hata Serikali ngazi ya mtaa, kijiji au kitongoji wao huuliza tu!
Una mri gani? Ukisema una miaka kumi na nane au zaidi hawafuatilii kutaka kujua
zaidi umri wako, kwahiyo wanalidhika na miaka utakayo waambia ndiomaana
ukitafuta kwa undani zaidi kiasi furani vijana wanao fanya kazi hapa kwenye
machimbo ni wana umri wa utoto.”
Kwamujibu
wa ofisi ya Ustawi wajamii Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Takwimu zinaonesha
kwamba zaidi ya watoto elfu saba (7000)
wanaishi katika mazingira hatarishi na idadi kubwa zaidi kati ya hao
hufanyishwa kazi zisizo za staha, zikiwemo za ugongaji kokoto na kwenye
machimbo.
Theresia Mwendapole ni afisa Ustawi wa
Jamii Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, alinieleza kuwa hali ya utumikishwaji
watoto kwenye maeneo ya machimbo, mashambani na kupasua kokoto bado ni tatizo,
wazazi nimojawapo ya sababu kubwa ya utumikishwaji huo hasa kwenye maeneo ya
machimbo ya dhahabu na kupasua kokoto, lakini pia wanao miliki mashimo ya dhahabu wakati mwingine huwatafuta vijana wakiume kwaajili ya kuwasaidia kazi, pasipo kufuatilia uhakika wa umri wao.
“Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Chunya mara kadhaa tunafanya ukaguzi kwen ye maeneo yote ya machimbo ambapo hua tukikuta utumikishwaji watoto tunawakamata wamiliki wa mashimo hayo, na kuwafikisha kwenye ngazi zinazohusika kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi” Alisema Theresia.
Umbali wa mita ishirini hivi (20mt) kutoka Shule ya Msingi Itumbi
kufika kwenye machimbo yajulikanayo kwa jina la ITUMBI nilipata nafasi ya
kufanya mahojiano na mwanafunzi mwenye uzoefu wa kazi za uchimbaji na
uchenjuaji madini anae Shuleni hapo, jinalake tunalihifadhi, “kwenye machimbo unaanza kidogo kidogo wakati mwingine unaenda na mzazi wako, mimi nilikuwa ninaenda na mama yangu kumsaidia kuchekecha mchanga wa dhahabu, ikafikia hatua mama akiwa haendi ninaenda mwenyewe kufanya kazi na pesa nilizo kuwa nikipata nampa mama yangu” alisema mwanafunzi huyo.
Utumikishwaji wa watoto kwenye migodi ni tatizo lenye athari za kielimu
katika eneo la Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya, kama ilivyo katika maeneo
mengine yanayokabiliwa na suala kama hilo, japokuwa wadau na Serikali
wanaendelea kupambana kutokomeza jambo hilo.
Watoto wengi wanashindwa kuendelea na masomo yao wanaposhawishika au
kulazimishwa kufanya kazi katika migodi, Hii inasababisha kukatishwa tamaa na
kuacha shule kabla ya kukamilisha elimu yao na kukosekana kwa elimu kunawaweka
katika hatari ya kukosa fursa za ajira bora baadaye maishani.
Amenye Kasambo ni Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Itumbi, iliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Chunya Mkoani Mbeya ameniambia sababu mojawapo zinazo sababaisha kuendelea kwa
utumikishwaji watoto maeneo ya machimbo, nakushindwa kutolipatia kipaumbele
suala la elimu kwa watoto wao. “Anasema wazazi na walezi hutumia watoto wao kwenye kazi za kutafuta kipato, wakazi huo bado niwafanzi jambo hilo ndio husababisha watoto kushindwa kuhudhulia Shuleni hatimae kuacha kabisa masomo”.
JE, SULUHISHO NI NINI ?
Ili
kukabiliana na tatizo la utumikishwaji watoto kwenye migodi, wadau mbalimbali mfano; Serikali, NGOs, Vyombo
vya habari na Wananchi wanapaswa kushiriki kikamilifu kwenye jamii na maeneo
ambayo yana hali na vitendo hivyo vya utumikishwaji wa watoto.
SERIKALI:
Kuweka na
kutekeleza sheria na kanuni kali zinazolinda haki za watoto na kuzuia
utumikishwaji kwenye migodi. Kuimarisha mifumo ya utekelezaji wa sheria na
kuongeza adhabu kali kwa wale wanaokiuka haki za watoto na Kuwekeza katika
elimu na kuongeza upatikanaji wa elimu bora ili kupunguza ukosefu wa fursa za
ajira na kuchochea maendeleo ya jamii.
NGOs (Asasi za
Kiraia):
Kufanya
kampeni za kuhamasisha umma na kutoa elimu kuhusu madhara ya utumikishwaji
watoto kwenye migodi, Kutoa msaada wa kisheria na kisaikolojia kwa watoto
walioathiriwa na utumikishwaji huo na kuwasaidia kupata fursa za elimu na
maendeleo na Kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kubuni na
kutekeleza mipango endelevu ya kuondoa utumikishwaji wa watoto kwenye migodi.
VYOMBO VYA HABARI:
Kuendeleza
uandishi wa habari unaolenga kuelimisha umma kuhusu utumikishwaji wa watoto
kwenye migodi na kushinikiza hatua za kukabiliana na tatizo hili, Kuangazia
visa vya utumikishwaji na kuwasaidia watoto kushiriki hadithi zao ili
kuhamasisha hatua za kuzuia na kuondoa utumikishwaji watoto kwenye migodi na Kutoa
jukwaa la mijadala na majadiliano kuhusu suluhisho na mbinu za kukabiliana na
tatizo hili.
WANANCHI:
Kushiriki
katika harakati za kupinga utumikishwaji watoto kwenye migodi kwa kuwajibika
kama wazazi, walezi na jamii kwa ujumla, Kuunga mkono miradi na programu za
kijamii zinazolenga kutoa fursa za elimu na maendeleo kwa watoto na familia
zinazoishi karibu na migodi na Kuwa walinzi na waangalizi katika maeneo yao na
kuripoti visa vya utumikishwaji watoto kwenye migodi kwa mamlaka husika.
MWALIMU MKUU:
Tatizo la
utumikishwaji watoto kwenye migodi linahitaji hatua za pamoja na ushirikiano
kutoka kwa wadau mbalimbali, kupitia jitihada za serikali, NGOs, vyombo vya
habari, na jamii kwa ujumla, tunaweza kuzuia athari mbaya za utumikishwaji huu
na kutoa fursa bora za maendeleo kwa watoto wetu.
Ni jukumu
letu kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao za msingi na wanakuwa na
mazingira salama na yenye ustawi bora, kwa kuunganisha nguvu tunaweza
kufanikiwa kuondoa utumikishwaji wa watoto kwenye migodi na kuunda ulimwengu
bora zaidi kwa kizazi kijacho.
Good article