hamasa kwa umma, wadau wa Elimu na Serikali kuchangia katika uboreshaji wa
Elimu nchini ikiwemo miundombinu ya Elimu na kuzingatia makundi maalumu kupata
Elimu.
Hayo yalielezwa na Mratibu wa kitaifa wa maadhimizo ya Juma la Elimu
Tanzania, Mkurugenzi wa Mtandao wa Elimu Tanzania –TEN/MET, Ochola Wayoga
katika uzinduzi wa Juma la Elimu uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi
Mvuha katika Kata ya Mvuha Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro vijijini.
“Maadhimisho haya yanatarajia kuongeza uelewa kwa umma, juu ya umuhimu
wa uchangiaji uboreshaji wa Elimu lakini namba mbili kuhamasisha Serikali
kuzingatia makundi yaliyokosa fursa kama watoto wenye ulemavu, watoto wa kike,
kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na lengo la Tatu ni
kuhamasisha na kukumbusha Jamii, Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
na wadau mbali mbali wa Elimu kuhumu umuhimu wa uchangiaji wa Elimu” alisema
Ochola Wayoga…
Katika Juma la Elimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro timu
ya TenMet kwa kushirikiana na Serikali ya Wilaya na wadau mbalimbali wa Elimu
ili kutambua changamoto za walimu na wanafunzi, walitembelea Shule walizopangiwa
na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, wakati huo huo wanamtandao wa TenMet walishiriki
katika shughuli nyingine zitakazobainika kulingana na uhitaji, pia walifanya
Vikao na kamati za Shule, walimu, wanafunzi, wazazi na wadau mbalimbali kwa
kuzingatia mada kuu yenye kaulimbiu isemayo, Tuboreshe uwekezaji wa rasilimali
za ndani kwenye Elimu kwa maendeleo endelevu.
Huu ni Mwaka wa 17 kufanyika maadhimisho ya Juma la Elimu nchini
Tanzania.
Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Juma la Elimu, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,
Rebecca Nsemwa aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alizungumzia eneo aina
ya rasilimali inayotakiwa kuwekezwa katika Elimu na jinsi Taifa linavyoweza
kuendelea.
Nchi yeyote ili iendelee inahitaji kuwekeza kwenye Elimu bora, Elimu
hiyo ni lazima itolewe kwa usawa wa kijinsia na jumuishi na kwa kuzingatia
mahitaji halisi ya wanafunzi, ili tufanikiwe ni lazima wadau wote wawajibike
katika nafasi zao na pia ili tufikie lengo la kuwa moja kat yka Nchi za kipato
cha kati hakuna budi Taifa Kuwekeza katika Elimu kwa watu wake na sehemu muhimu
ya kuanzia kuwekeza katika rasilimali watu ni Elimu ya awali na Msingi kwa watu
wote bila kuwaacha nyuma watoto wa kike” alisema Rebecca Nsemwa….
Kwa upande wake Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Mvuha, Elia Simon
anayesoma Kidato cha pili akihojiwa na Tanzania Kids Time alisema maadhimisho
ya Juma la Elimu kwao yanafaida kubwa kielimu na kuendeleza vipaji.
Elia Simon alisema “Maadhimisho haya yana sapoti katika maisha
ya Mwanafunzi kukuza vipaji, kwa mfano kwenye kuigiza, kujiamini na kujieleza
mbele ya watu kama walivyofanya walioongea kingereza, unajua mwanafunzi
anavyojifunza vile unajua kabisa huyu anajua hiki na hiki hakiwezi kwa hivyo
inasaidia kuwaelewa vizuri wanafunzi”…
Katika maadhimisho hayo ya Juma la Elimu, pia lilizinduliwa Darasa la
awali katika Shule ya Msingi Mvuha, ambalo ni Darasa linaloongea lenye vifaa na
zana mbali mbali za kusoma na kujifunzia kwa wanafunzi.
Akizungumzia Darasa hilo Mwalimu wa Shule hiyo, Rosemary Bundala
alisema “yani atakachojifunza Mwanafunzi kwanza ataipenda Shule, kingine
kiwango chake cha Elimu kitakua kwa mfano hili Darasa la awali linaloongea
ambalo limezinduliwa leo, lina zana nyingi za Mwanafunzi kujifunzia litaongeza
ari ya watoto kupenda Shule, watajifunza kwa kutumia Picha, maneo na zana zote
zilizomo kwake inakua rahisi kuelewa”.
Nchini Tanzania Juma la Elimu kitaifa limezinduliwa tarehe 17/4/2023
na linatarajia kufikia kilele tarehe 21/4/2023, katika Halmashauri ya Wilaya ya
Morogoro vijijini.
KWA NINI MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU
Maadhimisho ya Juma la Elimu (Global Action Week for
Education-GAWE) ni tukio la alama kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
yanayojishughulisha na Elimu duniani kote kama wito wa haraka na wenye nguvu
kwa Mataifa, viongozi wa ulimwengu na jumuiya ya kimataifa kulinda Elimu katika
Dharura na huadhimishwa kila ifikapo Juma la mwisho la mwezi wa Nne hadi wa
Tano kila mwaka tangu mwaka 2000.
TEN/MET INAVYOHUSIKA
KATIKA JUMA LA ELIMU.
TEN/MET ni mtandao wa kitaifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayojishughulisha na Elimu nchini Tanzania, hadi sasa TenMet ina wanachama
wapatao 184 nchi nzima. TEN/MET
inatazamia mfumo wa kitaifa wa Elimu ambao kila mtoto wa Kitanzania ana nafasi
ya kushiriki katika elimu bora, dira hiyo imetajirika kupitia dhamira yake ya
kuratibu na kuimarisha asasi za kiraia nchini Tanzania kupitia mitandao,
kujenga uwezo, utafiti na utetezi.
Kwa miaka 17 sasa TEN/MET kwa kushirikiana na serikali na
wadau wengine wa Elimu nchini wamekuwa wakishiriki kutimiza wito wa kuadhimisha
Juma la Elimu (Global Action Week for Education-GAWE) nchini Tanzania.
Soma zaidi kuhusu TenMet: https://tenmet.or.tz/about-us/