Leo ikiwa nisiku ya mtoto wa Africa,maadhimisho haya mwaka huu yataadhimishwa tofauti na miaka mingine yote iliowahi kupita.
Kaulimbiu mwaka huu ina sema,”Mifumo rafiki ya Upatikanaji Haki za Mtoto; Msingi Imara wa kulinda haki zao”. Makamu mwenyekiyi wa baraza la watoto mkoa wa morogoro ameonyesha masikitiko yake kuhusu kutofanyika maadhimisho haya kama ilivyo kawaida na siku miaka mingine.
“Kwa majina naitwa Paulina Anolas mimi ni makamu mwenyekiti wa baraza la watoto mkoa wa Morogoro. Kama ilivyo ada kila ifikapo tarehe 16 mwezi wa 6 huwa tunaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika katika maadhimisho hayo watoto huwa tunakaa pamoja na kufanya mambo mbalimbali kama watoto.Kutokanana janga hili la covid 19 kuikumba dunia tunasikitika kwa kusema mwaka huu tumeshindwa kufanya hivyo. Hata hivyo niwatakie watoto wenzangu maadhimisho mema wakiwa huko majumbani asante“.
Aidha mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Tanzania Anna Henga amebainisha mambo walio yabaini kwa kipindi cha miaka mitatu (3) iliopita kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
“ Kwa kipindi cha miaka mitatu iliopita haki ilio vunjwa nihaki ya mtoto na matukio mengi yaliwahusu watoto,hasa ya kiwa ni ukatili wa kingono, hivyo tunavyo adhimisha siku hii ya mtoto wa Afrika nilazima tuangalie yunawalindaje watoto wetu”.
Kwa upande wa vituo vya kulelea watoto ugonjwa huu wa Covid-19 ume wa athili namna gani kuwatunza watoto pasipo posho yeyote wanayo pata kutoka kwa wazazi,walezi au wadau maendeleo ya watoto kwa kipindi cha miezi mitatu sasa inaenda kuisha.
Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika bi, Caroline Makemo yeye anakituo cha kulelea watoto kilichopo Dumila wilaya ya kilosa Morogoro,amepaza sauti yake kwa jamii “Ninao watoto ninakaa nao pale mkubwa kabisa ana miaka kumi na mbili na mdogo ana miaka miwili,na akatoa wito kwa jamii kusaidia chochote ilikuunga mkono maendeleo na ustawi wa mtoto”.