SHAIRI KUHUSU SIKU YA MTOTO WA AFRIKA:
1.Mnamo mwaka 1976 June huko Soweto
Kulipiganwa Vita vikali na Watoto
Hakuna alieamini kwani ni kama ndoto
Walijitolea muhanga ili kuiondoa changamoto.
Ya kufundishwa kwa kutumia lugha yao
Na wakawa tayari kuhatarisha maisha yao.
2.Leo ni siku muhimu ambayo tunaadhimisha ,ili kuwaenzi Watoto wenzetu kwa kuwawakilisha
Kwanza tumshukuru mungu uhai kutufikisha
Siku hii adhima kuweza kuadhimisha
3.Tunahuzunika kwa siku hiii hakika
Furaha nyingi tunazo ila sasa zimekatika
Kwani hatutopata kuadhimisha siku hii kwa kukusanyika
Hakika korona imetubana vurugu patashika
4.Ila mwaka huu tunaadhimisha online
Na wala hatujafurahiya
Wasiwasi wetu je? Watafurahia wenzetu
Waliopambania
Bila ya kujali muhanga kujitoleya
Kwa kutaka haki zetu zilindwe mpka mwisho Wa dunia
5.Ili tufurahike Watoto sote Wa Afrika tukusanyike
Bila ya kujali mwanaume au mwanamke
Ili kuhakikisha haki zetu tuzipate
Ila mwaka huu kila mtoto yumpweke
Hakika korona inatufanya tunyanyasike
6.Nilieandika shairi hili ni mwenyekiti Wa Barza la Watoto
Ili kuonesha jinsi gani korona imetupa changamoto
Katika siku hii ya kuadhimisha siku ya mtoto
Natoa shukran za dhati kwa serekali na mashirika ya binafsi
Licha ya uwepo Wa korona ila bado mupamoja nasi .
15/6/2020
Asiya Makame
Chairwoman of Ncab.