Mkurugenzi wa Huduma ya Vijana Kusini mwa Tanzania katika kanisa la Waadvenyista Wasabato, Mchungaji Joseph Dzombe ameahirisha zoezi la huduma ya Matendo ya huruma, yaliyoanza Machi 15 hadi Machi 21 ambayo yalijikita kuwasaidia wahitaji kwa kutoa misaada mbalimbali, kwa ajili ya tahadhari ya Ugonjwa wa Corona (COVID 19).
Hayo yamekuja baada ya kutolewa kwa Waraka wa kutaka kuahirishwa kwa zoezi la matendo ya huruma kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma ya Vijana Ulimwenguni Mchungaji Gary Blanchard na badala yake kuendelea na wiki ya maombi kwa kuiombea Dunia na kujifunza neno la Mungu.
Aidha Mchungaji Dzombe amewataka waumini kujikita katika maombi ya kuliombea Taifa ili kulinusuru na janga la ugonjwa wa Corona huku akiwasisitiza kuendelea kutenda matendo mema katika jamii pamoja na kufanya kazi kwa bidii.
“wiki ya matendo ya huruma yameahirishwa hadi hapo yatakapotangazwa tena, tuendelee kujikabidhi kwa Mungu tukiamini anaweza kutuepusha na balaa hili la ugonjwa wa COVID 19 na tuwaombee waliopatwa wapone haraka” amesema.
Pia Katibu wa Idara ya Vijana Mtaa wa Misufini Daniel Ngofira ameiomba jamii kuendelea kuwaombea watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kwani Machi 21, 2020 vijana hao walipanga kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Kauzeni iliyopo manispaa ya Morogoro vikiwemo vifaa mbalimbali vya Shule.
“tulipanga kuwasaidia watoto katika shule ya kauzeni, kwani wapo wanajamii wanowasaidia si kama wazazi wao hivyo nasi tulipanga machi 21 kutoa msaada kwao ili waweze kuzifikia ndoto zao” amesema.
Hata hivyo kabala ya kutolewa kwa tamko la kuahirisha zoezi la matendo ya huruma, ili kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona, huku Machi 15,2020 vijana hao walisafisha maeneo mbalimbali ya hospitali ya Mafiga na kutoa msaada kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya Matendo ya Huruma.
MOROGORO
Shua Ndereka.
Congrats; Keep it up!!!