Wadau wa elimu wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wameombwa kujitokeza kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwawezesha kufikia malengo yao.
Hayo yamebainishwa na mwanzilishi wa huduma ya Niwezeshe ni Fikie Malengo Ndg, EDGA DONALD SAHARI, katika mahojiano maalumu na TKT/UN RADIO amesema huduma hiyo ilianzishwa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu pindi wazazi wao wanapokuwa wamefariki na kubaki na walezi wasiokidhi huduma za watoto hao.
Aidha mjumbe wa huduma hiyo bwana SITA BAKARI pamoja na walezi wa watoto hao wameelezea kwa pamoja mazingira walio nayo kwa hivi sasa ni pamoja na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo chakula, vifaa, vya shule na kuwaomba wadau kujitokeza kuwasaidia watoto hao ilikufanikisha malengo walio nayo japo wengine hawana wazazi wao.
Hata hivyo Jenipher Abery na Samweli Matona wao wanasoma darasa la tano shule ya msingi Nyamililo wameelezea adha wanayoipata pindi wawapo shuleni,hasa wanapo waona wenzao wana vifaa vipya vya shuleni kamavile Daftari,Sale,viatu na kubwa zaidi kushinda na kulala njaa nyumbani kwao, tangu mwaka jana hatukufanikiwa kununuliwa nguo mpya, tumeanza shule mwaka huu shule wengi wetu hakuna vitu vipya hata daftari,tunaiomba kwa yeyote atakae guswa atusaidie hata kutununulia daftari.
Wadau wakishirikiana kwa pamoja kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu itaweza kuwainua kitaaluma na kuongeza ufaulu kaika masomo yao ili kufikia kutimiza ndoto zao.
Na Deborah/mhariri mgozi