huyo Abdel Razzaq mwenye umri wa miaka 12 aligunduliwa kipaji hicho na
Profesa Abbas Maana kupitia mradi wa kufundisha watoto unaondeshwa na
shirika la kiraia la Teach For Lebanon.
mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR,
Profesa Maana ambaye amekuwa anatembelea nyumbani kwa mtoto Razzaq
anasema..
“Mara ya kwanza nilipokutana na Abdel niliweza kufahamu alikuwa na uelewa mkubwa. Alikuwa na akili, lakini alikosa kujiamini”
Teach For Lebanon, shirika ambalo linasaidia elimu katika shule
nchini Lebanoni tayari limesaidia kuelimisha zaidi ya watoto 5000 wa
Lebanon na Syria ambapo Profesa Maana anasema..
“Bila kujali utaifa wa mtoto au hali yake ya awali, tunataka kuangazia uwezo wa mtoto na kuongeza uwezo wa stadi alizonazo.”
Azma hii inaonekana kutimia kwa mtoto Abdel ambaye kipaji chake kingeweza kupotea bila kufahamika Profesa Maana..
“Nimejifunza kutoka kwa Profesa Abbas maadili mengi ikiwamo
kutokata tamaa na kuwasaidia wengine. Ndoto yangu ni kukua na kuwa
mwanasayansi kuvumbua dunia inayonizunguka.”
Lebanon inahifadhi watoto wakimbizi waliosajiliwa wapatao 987,000
kutoka Syria ambapo kati yao hao 490,000 ni watoto wenye umri wa kwenda
shule kuanzia umri wa miaka mitatu hadi 18.
UNHCR inasema kuwa watoto wakimbizi 220,000 wanasoma na wenzao wa
Lebanon katika shule za umma asubuhi au madarasa ya jioni mahususi kwa
watoto wasyria walioko ukimbizi Lebanoni.
Taarifa hiin nikwa mjibu wa radio washirika UN RADIO.