Mkutano maalum unafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa mjini New
York Marekani ili kujadilia mbinu muafaka za kusaidia kuwajumuisha katika
jamii watoto walioshiriki migogoro ya silaha na kuepusha migogoro zaidi.
Lengo la mkutano huo uliowaleta pamoja wadau mbalimbali akiwemo mwakalishi
wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye migogoro ya silaha ni
kutathmini mpango wa miaka mingi wa kupigania haki za watoto ambao
wamekuwa wanahusishwa katika migogoro ya silaha dunaini pasipo ridhaa yao.
Mbinu hizo zitawasaidia watoto hao kuweza kuishi maisha
salama na kukubalika na changamoto katika jamii baada ya kushiriki
katika migogoro.
Mmoja wa askari watoto wa zamani akiwa na umri wa miaka kumi na miwili tu alipojiunga
vitani ni Alfred Orono Orono,hivi sasa ni afisa anaehusika na
kuwalinda watoto katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani nchini
Sudan Kusini UNMISS nae aeleza athari za watoto kushiriki migogoro
ya silaha
Mazungumzo haya pia yana nia ya kutoa picha kamili
ya kampeini hiyo kuwajumuisha watoto katika jamii ambayo
imedumu miaka mitano pamoja na umuhimu wake na jinsi unavyosaidia maisha
ya watoto ambao zamani walikuwa wanabeba bunduki ambao unawasaidia, Taarifa hii nikwa mjibu wa radio ya Umoja wa Mataifa UN RADIO New York Marekani.