Watoto 55,000 wanakadiriwa kuwa katika hatari kubwa ya mafuriko na
maporomoko ya udongo kwenye makazi ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh
limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Japo msimu rasmi wa mvua na pepo za Munsoon haujaanza ,Kwa mujibu wa UNICEF
mvua za awali zimeanza na kuleta athari kwenye makazi hayo ya Cox’s Bazaar eneo
linalotambulikwa kwa kukumbwa na mafuriko kila mara.
Mvua hizo ambazo zimeanza kunyesha tarehe 27 zikiambataza na kimbunga ,
kufikia leo zimeshaathiri maelfu ya familia na wakimbizi Cox’s Bazaar
wengi wakiwa ni watoto walioonekana kupanda juu ya paa za plastiki za makazi
hayo ili kujaribu kuzuia upepo kuyaezua. Christopher Boulerac ni
msemaji wa UNICEF Geneva
“Tunakadiria zaidi ya watu 100,000 wakiwemo
watoto 55,000 , wako katika hatari kutokana na mafuriko na maporomoko ya
udongo, inawezekana idadi hiyo ikafika hata 200,000 kutegemeana na ukubwa wa
mvua.”
Ameongeza kuwa ingawa msimu ramsi utaanza Juni hali hii inadhihirisha ni
jinsi gani msimu huo utakavyokuwa na athari kwa maelfu ya wakimbizi, Hii
nikwamjibu wa Radio ya Umoja wa mataifa UN news.