Ukeketaji wa watoto wa kike na
wanawake unasalia kuwa ni jambo linalotishia tu siyo afya ya kundi hili bali
pia maendeleo yao ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Sasa watoto wenyewe wa kike
wanasimama kidete kuhakikisha hawakumbwi na kikwazo hicho.
Harakati za kuondokana na ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake , FGM,
zinazaa matunda pale msichana anapopaza sauti na jamii yake kuitikia.
Hiyo imekuwa dhahiri kwa Purity Soinato Oiyie, msichana wa kimasai kutoka
Kenya ambaye akiwa na umri wa miaka 11 alikwepa kitendo hicho haramu,akihojiwa
na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Purity
amesimulia alifanikiwa vipi kukwepa mkono wa ngariba.
Hivi sasa Purity mwenye umri wa miaka
22 amefanikiwa kuhitimu shahada yake ya kwanza ya Chuo Kikuu akijikita katika
masuala ya elimu. Pamoja na kwamba ni mjumbe wa Bodi ya kitaifa nchini Kenya ya
kukabiliana na FGM, Purity hutumia muda wake mwingi kuhamasisha wasichana na
jamii dhidi ya , ukeketaji. Je mwitiki uko vipi? Taarifa hii ni kwa mjibu wa UN
Radio.
https://news.un.org/sw/story/2018/04/1010521?utm_source=UN+News+-+Kiswahili&utm_campaign=d0fde00026-EMAIL_CAMPAIGN_2018_04_05&utm_medium=email&utm_term=0_36307a21c7-d0fde00026-105232733