Na, John Kabambala:
Muuguzi mmoja mahiri katika hospitali ya
Taifa Muhimbili. Alikuwa na shauku kubwa ya kuokoa maisha ya watoto njiti.
Tangu utoto wake, alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi na kuwasaidia watoto wadogo
kuanza maisha yao vizuri. Sasa, akiwa na uzoefu wa miaka kadhaa, alikumbushwa
kila siku kuhusu ndoto yake alipoona watoto njiti wakipambana na changamoto za
maisha.
Mmoja wa wagonjwa wake alikuwa Amina, mtoto njiti mwenye
uzito wa chini sana aliyezaliwa wiki sita kabla ya muda. Amina alikuwa na
mapigo ya moyo dhaifu na matatizo ya kupumua, na hali yake ilikuwa tete, mbali
na hali hiyo alijitolea kwa moyo wote kumuokoa.
Alianza kwa kumfanyia Amina uchunguzi makini na kugundua matatizo
kadhaa. Kwa umakini wa hali ya juu, alimshughulikia kwa uangalifu, akimtunza na
kumpatia lishe bora kupitia njia ya mishipa. Alisimamia viwango vyake vya
oksijeni na alimhudumia kwa upendo na kujali, akimfariji na kumtia moyo mama
yake, Fatma, ambaye alikuwa na wasiwasi mkubwa.
Muuguzi huyu alifanya kazi kwa karibu na timu ya wauguzi na
wataalamu wengine wa afya ili kutoa huduma bora kwa Amina. Walifanya kila
wawezalo kumwezesha kupumua vizuri na kupona. Pamoja na changamoto nyingi
lakini hakukata tamaa. Aliendelea kufuatilia maendeleo ya Amina kwa karibu na
kufanya marekebisho ya matibabu kadri ilivyohitajika.
Baada ya wiki kadhaa za mapambano na matibabu ya kujitolea,
Amina alianza kuonyesha dalili za kuimarika zaidi. Mapigo ya moyo yalikuwa
thabiti, na alianza kupumua vizuri zaidi. Muuguzi huyu kwa kushirikiana na timu
yake walifurahi sana kumuona Amina akianza kuchanua na kuongezeka uzito.
Hatimaye, siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ilifika – Amina aliweza kuondoka
hospitalini akiwa na afya njema.
Muuguzi huyu alikuwa
na furaha kubwa kuona ndoto yake ikitimia. Alijawa na furaha kuwa
sehemu ya maisha ya Amina na familia yake. Kwa bidii, ujuzi, na upendo, alikuwa
amepambana na kushinda changamoto kubwa ya kuokoa maisha ya mtoto njiti. Kwenye
makala hii leo tunamzungumzia Nay Mollel yeye ni muuguzi kutokea
hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Pamoja na kazi yangu ya uuguzi ya kuwahudumia wazazi
wengine wenye watoto ambao walizaliwa kabla hawajakomaa, mimi pia nimejifungua
watoto wa aina hiyo, kiukweli niliogopa kwa kiasi kikubwa kuona hali ile ambayo
nilizoea kuiona kwa wazazi wengine tu, lakini mume wangu na mama yangu mzazi
alinitia moyo sana familia nzima ikaondoa mawazo ya kuona ni watoto waliozaliwa
kabla ya muda wao sahihi, wakuzaliwa bali mawazo yalihamia kufurahia uwepo wa
mapacha” huyo ni Nay Mollel muuguzi katika hosipitali ya taifa ya Muhimbili.
Mwishoni mwaka 2022, shirika la afya duniani WHO limezindua muongozo mpya wa
kuboresha uhai na matokeo ya kiafya ya Watoto wanaozaliwa kabla ya wiki 37 au
wenye uzito wa chini ya kilo mbili na nusu wakati wa kuzaliwa.
Muongozo huo uliozinduliwa mjini Geneva Uswis unashauri mfumo wa Ngozi kwa
Ngozi baina ya mtoto na mlezi alimaarufu kama kangaroo na unapaswa kuaanza
punde mara baada ya mtoto kuzaliwa.
TATIZO LA KUJIFUNGUA WATOTO AMBAO HAWAJAKOMAA:
Tatizo hili la watoto wanaozaliwa kabla ya kutimiza umri wa wiki 37 liko
duniani kote, lakini zaidi sana ni nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ndio
zinawatoto wengi ikiwemo Tanzania.
Kwa Bara la Afrika, Nigeria ni nchi inayo ongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya
watoto waliozaliwa mimba imekomaa, wakati nchi ya Tanzania ina asilimia kubwa
ya watoto wanaozaliwa kabla ya mimba kukomaa.
Miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha mama kujifungua watoto ambao
hawajatimiza umri wa mimba kukomaa ni pamoja na magonjwa kama vile, kifafa cha
mimba tatizo linalosabishwa na shinikizo la damu wakati wa ujauzito, maambukizi
ya vimelea vya bacteria katika njia ya mkojo yaani UTI, kutangulia kwa kondo la
nyuma, mimba za mapacha za watoto wawili na kuendelea na mimba za utotoni
nimiongoni mwa sababu.
Nime zungumza na Daktari Bingwa Mbobezinwa watoto wachanga, kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Martha Mkony amesema nchini Tanzania Mkoa unaongoza kuwa na
watoto wengi kwa kila siku waliozaliwa kabla mimba haijakomaa, ni Dar es Salaam
ikilinganishwa na mikoa mingine nchini Tanzania.
Aidha Dr. Mkony amesema tangu mwaka 2008 alipo ingia kwenye kitengo cha watoto
wachanga walikuwa wakilaza wastani wa watoto 20 waliozaliwa kabla ya wakati kwa
kila siku, ambapo idadi hii imepungua zaidi ya 50% kwa sababu ya juhudi za
Serikali kuboresha huduma za afya kwa wajawazito na watoto wachanga katika
ngazi zote nchini, ikiwa ni pamoja na kusomesha wataalam katika fani hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “Watoto wanao
zaliwa kabla ya wakati wanaweza kuishi, kushamiri na kubadili dunia , lakini
kila mtoto lazima apewe fursa. Muongozo huu mpya unaonyesha kwamba kuboresha
matokeo ya Watoto hawa ambao hawaja komaa, sio kila wakati ni kuhusu suluhu za
teknolojia ya hali ya juu, bali ni kuhakikisha fursa ya huduma muhimu za afya
ambazo zinakwenda sanjari na mahitaji ya familia.”
CHANGAMOTO KUBWA YA WATOTO HAWA:
Changamoto kubwa inayo wakumba watoto waliozaliwa kabla mimba haijakomaa, ni
tatizo la upumuaji, mapafu ya watoto hawa unakuta hayajakomaa kuweza kusaidia
mfumo wa upumuaji kufanya kazi yake ipasavyo.
Nay Mollel ni Mama aliejifungua watoto ambao hawajatimiza umri wa kuzaliwa uzao
wa kwanza na uzao wapili, na pia kitaaluma ni Muuguzi na nimuajiliwa wa
Serikali katika hospital ya taifa ya Muhimbili, ananieleza kwa mara ya kwanza
hali ilikuwaje alipojifungua watoto mapacha ambao hawajatimiza umri wao wa
kuzaliwa.
“Pamoja na kazi yangu ya uuguzi ya kuwahudumia wazazi wengine wenye watoto
ambao walizaliwa kabla hawajakomaa, mimi pia nimejifungua watoto wa aina hiyo
japo sikuwahi kutegemea kuwa nitajifungua watoto wa aina hiyo.
Na kiukweli niliogopa kwa kiasi kikubwa kuona hali ile ambayo nilizoea kuiona
kwa wazazi wengine tu, lakini mume wangu na mama yangu mzazi alinitia moyo sana
familia nzima ikaondoa mawazo ya kuona ni watoto waliozaliwa kabla ya muda wao
sahihi, wakuzaliwa bali mawazo yalihamia kufurahia uwepo wa mapacha”.
Katika kuwahudumia watoto hawa nilijitahidi sana kuwabeba ngozi kwa ngozi na
kuwanyonyesha maziwa ya mama bilakuwa changanyia maziwa mengine kabla yakufikia
muda walio ushauri madaktari bingwa wa watoto, na nilifanikiwa kuwakuza na sasa
wana umri wa miaka kumi na tatu (13), na wanasoma kidato cha kwanza.
Aidha Bi, Mollel anasema “nilipo beba ujauzito mwingine nilipata shida ya
kuvuja damu kwa muda mrefu, hali ile ilisababisha nifanyie upasuaji ilikumuokoa
mtoto aliopo tumboni japo muda wa kuzaliwa ulikuwa bado haujatimia” hadi sasa
bi, Mollel ana watoto watatu wawili wakike mmoja wakiume wote walizaliwa kabla
mimba haijakomaa.
UZOEFU WA MALEZI YA WATOTO AMBAO HAWAJAKOMAA:
Hata hivyo Nay Mollel anaeleza uzoefu wake katika kuwalea watoto ambao wanazaliwa
kabla mimba haijakomaa, maziwa ya kuwakuza nigharama kubwa na ukizingatia
watoto wangu walikuwa mapacha hivyo kopo moja 1 la maziwa walikuwa wakitumia
kwa siku mbili linaisha, hivyo kama mzazi ambae kipato chake ni cha chini zaidi
hupata mtihani mkubwa wa kuwahudumia katika kipindi chote cha unyonya.
Jambo lingine anasema ni likizo ya uzazi, kwa mujibu watartibu za kazi Mama
akijifungua hupewa likizo ya uzazi ya siku 84 na muajili wake, likizo hiyo ni
kwa Mama ambae amjifungua kawaida na mtoto wake hana shida yeyote, lakini kwa
Mama ambae amejifungua mtoto kabla ya mimba haijakomaa bado hana likizo yake
maalum kulingana na hali ya malezi ya mtoto au watoto wake hadi kufikisha uzito
unaotakiwa, hiyo ndio changamoto wanayo kumbana nayo wakina mama wengi
waliojifungua watoto ambao hawajakomaa.
Dr. Martha Mkony anasema huu sio mkosi kwa familia, kama ambavyo baadhi ya watu
hudhani, jambo ambalo sio sahihi, jamii inapswa kufahamu kuwa jambo hili laweza
kutokea kwa wakati wowote na kwa Mama mjamzito yeyote, na kwa upande wa
Serikali kunahaja ya kuongeza muda wa likizo ya uzazi kwa Mama anaejifungua
mtoto ambae mimba haija timiza muda wake, kuliko ilivyo sasa.
Nini kifanyike, Serikali iweke utaratibu wa kisheria juu ya likizo ya uzazi kwa
Mama anaejifungua mtoto ambae mimba haija timiza muda wake, lakini pia Serikali
iongeze ruzuku kwenye vifaa na maziwa yanayo saidia kuwakuza watoto waliozaliwa
na hawajakomaa, ilikuwapunguzia mzigo na msongo wa mawazo wazazi wenye kipato
cha chini, mbali na hilo Bi, Mollel anaseama vifaatiba viongezwe vinavyo
wasaidia watoto wanao zaliwa kabla ya wakati ilikupunguza vifo dhidi yao.
MTAZAMO WA WABUNGE KWENYE KIKAO CHA TISA MWAKA HUU:
Katika kikao cha tisa cha bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Shally
Raymond mbunge wa viti maalum kutoka Mkoa wa Moshi anitaka Serikali ilipie bima
ya matibabu ya afya kwa watoto wanao zaliwa kabla ya wakati, ilikuwapunguzia
wazazi mzigo wa gharama za kifedha wanaojifungua watoto kabla yakutimiza umri
wao wa kuzaliwa.
Kwa upande wake Zainab Katimba mbunge wa viti maalum kutoka Mkoa wa Dar es
Salaam, anaiomba Serikali ifanye marekebisho ya Sheria ya likizo, kwa mwanamke
anaejifungua mtoto ambae mimba haijafikisha mudawake aongezewe likizo ya uzazi,
ili kumlea mtoto wake hadi kipindi atakacho komaa.