Na, John Kabambala:
Mwaka 2013, Tanzania ilishuhudia mwanzo wa mabadiliko
makubwa katika elimu ya msingi na sekondari kupitia mradi wa kusisimua
ulioanzishwa na Shirika la CAMFED (Campaign for Female Education). Mradi huu
ulikuwa na lengo la kuboresha stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike na kuwapa
fursa zaidi za elimu na ujifunzaji. Makala ya mradi huu inaanza na jitihada za CAMFED
kuleta mabadiliko chanya katika elimu na maisha ya wanafunzi wa kike nchini
Tanzania.
Kwa muda mrefu, wanafunzi wa kike nchini Tanzania wamekutana
na changamoto nyingi katika kupata elimu bora na kufikia malengo yao ya elimu.
Hali hii ilitokana na sababu kama vile umaskini, mila na desturi potofu, na
upungufu wa rasilimali za elimu. CAMFED, ni shirika la kimataifa linalofanya kazi katika
nchi kadhaa za Afrika, lilichukua hatua kwa kushirikiana na serikali ya
Tanzania na wadau wengine kuanzisha mradi wa Stadi za Maisha kwa Wanafunzi wa
Kike kwenye shule za Sekondari.
Sophia Leonard
yeye nimnufaika wa program mbalimbali zinazo wezeshwa na Shirika la Camfed
Tanzania, na amepata mafunzo na kuhitu ya kuwa muwezeshaji wa Stadi za Maisha
kwa vijana Shuleni, anasema kupitia elimu anayo wafundisha vijana shuleni tangu
Mwaka 2014 kwa zaidi ya miaka nane (8)
kwenye Shule ya Sekondari “KUTUKUTU”
iliopo Wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro . Sasa Wlimu, Ofisi za Elimu na Jamii zinashekhlekea
mavuno mazuri ya elimu hiyo ya Stadi za Maisha kwa watoto wao, Maana kiwango
cha taaluma kimeongezeka kuliko ilivyo kuwa kabla.
ELIMU YA STADI ZA
MAISHA KWA VIJANA HUCHOCHEA NINI HASA?
Kuandaa Wanafunzi kwa Maisha Baada ya Shule:
Elimu ya stadi za maisha inawasaidia wanafunzi kuwa tayari
kwa maisha baada ya kumaliza masomo yao. Kupitia kujifunza stadi za maisha kama
vile ujasiriamali, uongozi, ujuzi wa kujitegemea, na mawasiliano, wanafunzi
wanaweza kuwa na uwezo wa kufanikiwa katika kazi zao na kuchangia katika
maendeleo ya taifa. Na Serikali inapaswa kusimamia ili kuhakikisha kuwa
wanafunzi wanapata mafunzo haya muhimu katika shule za sekondari.
Kujenga Jamii yenye Ujuzi na Ubunifu:
Stadi za maisha hufundisha wanafunzi jinsi ya kutatua
matatizo, kuwa wabunifu, na kuwa na uwezo wa kubadilika katika mazingira
mbalimbali. Kwa kusimamia elimu hii, serikali inaweza kusaidia kuunda jamii
yenye watu wenye ujuzi na ubunifu, ambao wanaweza kuchangia katika kukuza
uchumi na kuleta mabadiliko chanya katika nchi.
KUHUSU CAMFED, TANZANIA NA MALENGO YA DUNIA (SDGs):
Kupunguza Umaskini na Ukosefu wa Ajira:
Nchini Tanzania, kama yalivyo maeneo mengine duniani,
ukosefu wa ajira na umaskini ni changamoto kubwa. Kwa kuwapa wanafunzi Elimu ya stadi za maisha, serikali inaweza
kuwasaidia kuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe au kushiriki katika shughuli za
uzalishaji kwa muda mfupi baada ya kumaliza masomo yao. Hii inaweza kupunguza
ukosefu wa ajira na kusaidia kupunguza umaskini katika jamii.
Kuimarisha Maadili na Uongozi:
Elimu ya stadi za maisha pia inajumuisha mafundisho ya
maadili na uongozi. Wanafunzi wanajifunza jinsi ya kuwa raia wema na viongozi
bora katika jamii. Kwa kuwekeza katika elimu hii, inaweza kuchangia katika
kujenga jamii inayozingatia maadili na uongozi wa heshima.
Kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs):
Tanzania, kama sehemu ya jumuiya ya kimataifa, imejiunga na
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Baadhi ya malengo haya yanahusu elimu na
ustawi wa jamii kama vile lengo No. 4
na 5. Kusimamia elimu ya stadi za
maisha ni njia mojawapo ya kuchangia katika kufikia malengo haya, kama vile
kuboresha elimu kwa wote, kukuza usawa, na kuhakikisha maisha bora na usawa wa
kijinsia.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa washirika hilola Camfed nchini
Tanzania Bi, Nasikiwa Duke anasema
wakati mradi huo wa Stadi za Maisha unaanza walizifikia Shule 365 za Sekondari lakini hadi kufikia
mwaka huu wamezifikia Shule 466,
ambazo zina nufaika na program ya Stadi za Maisha.
“CAMFED
iliwezesha elimu ya mafunzo ya stadi za
maisha kwa wanafunzi wa kike ili kuwajengea ujuzi wa kujitegemea, kujitambua,
na kushiriki kikamilifu katika jamii. Hii ililenga kuwawezesha kuwa viongozi na
wabunifu katika maisha yao. Na ilifanya kwenye jamii ili kubadilisha mtazamo wa
jamii kuhusu elimu ya kwa watoto wa kike na kuondoa mila na desturi potofu
zinazoweza kuzuia upatikanaji wa elimu kwa wasichana” Alisema
bi, Nasikiwa Duke.
Kwa upande wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,
Nilimuuliza Ndg.Mussa Mnyeti nikwa namna gani Program hii ya Stadi za
Maisha kwa wanafunzi ina umuhimu kwa Serikali?
“Programu hii inachochea
maeneo kadhaa ikiwemo kukuza Uongozi na Ujifunzaji, na inasisitiza uendelezaji
wa uongozi na ujifunzaji wa wanafunzi wa kike kupitia kwa walimu walezi na
vikundi vya wanafunzi Shuleni. Hii imeendelea kusaidia kujenga ujasiri na uwezo
wa kushiriki katika masuala ya elimu na kijamii kabla na baada ya kuhitimu
masomo yao ya elimu ya Sekondari.
Programu hii ya Stadi za Maisha ni mkakati unaoisaidia
Serikali kupambana na mdondoko kwa wanafunzi hasa wakike, kwani kumekuwepo na
changamoto nyingi zinazo wakumba watoto wakike ikiwa ni pamoja na kukatisha
masomo kwa sababu ya mimba za utotoni na changamo za kimazingira.
Hivyo kupitia mpango huu ambao unahusu kuwafundisha vijana
Stadi za Maisha wakiwa bado shuleni, ninaamini kabisa Serikali inauunga mkono,
na kumuandalia mazingira mazuri kwa watendaji kazi ilikwamba mdau huyu wa elimu
ambae ni Camfed aweze kufikia shabaha ilio kusudiwa” Alisema Ndg. Mnyeti.
Kupitia jitihada hizi, za Stadi za Maisha ziliwezesha
mabadiliko makubwa katika maisha ya wanafunzi wa kike nchini Tanzania.
Wanafunzi wengi wa kike walipata fursa ya elimu bora na kujifunza stadi muhimu
za maisha ambazo zilikuwa muhimu katika kujenga mustakabali wao. Pia, program hii
iliongeza uwepo wa wanawake katika nyanja za uongozi na uvumbuzi.
Matokeo chanya yalio tajwa na mkurugenzi wa shirika la
Camfed Tanzania yanathibitishwa na Mkuu wa divisheni ya Elimu Sekondari kutoka
halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Bi,
Salama Ndyetabura ambapo anasema kupitia ofisi yake imefanikiwa kurejesha
wanafunzi walio kuwa wamekatiza masomo kwa sababu mbalimbali, kamavile mimba za
utotoni, mazingira magumu na kwa sababu ya mifarakano ya wazazi.
“Kupitia program ya Stadi
za Maisha shuleni imefanikisha wanafunzi wengi kujitambua na kuchochea ufaulu
mkubwa kwa wanafunzi, hasa katika idara ya elimu Sekondari katika halmashauri
ya Chalinze. Kwa mujibu wa malengo ya program hii ya Stadi za Maisha kwenye
Shule za Sekondari nchini shirika kwa kushirikiana na Seriikali linatarajia
kufikia asilimia 85% ya Shule zote ifikapo mwaka 2030, ikiwa nimoja ya njia ya kuunga mkono Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya kudumu ya Umoja
wa Mataifa SDGs.
Serikali ina jukumu kubwa la kusimamia elimu ya stadi za
maisha katika shule za sekondari nchini Tanzania. Kufanya hivyo kutachangia
katika kuandaa wanafunzi kwa maisha baada ya shule, kuimarisha uchumi,
kupunguza umaskini, kukuza maadili na uongozi bora, na kufikia malengo ya
maendeleo endelevu. Ni muhimu kwa serikali kuwekeza katika rasilimali na sera
za kuboresha elimu hii ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata stadi za
maisha muhimu kwa maendeleo yao binafsi na ya taifa kwa ujumla” Alisema Bi, Salama Ndyetabura.