Picha kutoka unnews.
Na, John Kabambala.
Nukuu muhimu ambayo unapaswa kuendelea kuimbuka kupitia usomaji wa
makala hii ni kwamba: “Kila mtoto njiti ana thamani na uwezo
wa kipekee.” Kwani “Kila
mtoto njiti ni kipande cha hazina kwenye jamii yetu.” Kuzaliwa kwa
mtoto njiti ni changamoto inayohitaji upendo, ujasiri, na msaada kutoka kwa
familia, jamii, na serikali. Mtoto njiti ni mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati
au na uzito wa chini kuliko wastani. Hali hii inaweza kuwa ya kusumbua na
kutisha kwa wazazi hasa kwa wale ndio uzao wao wakwanza, lakini inatoa fursa ya
kipekee ya kuonyesha nguvu ya upendo na ujasiri wa binadamu.
“Mtoto
njiti, mara nyingi huwa na matatizo ya kiafya yanayohitaji uangalifu wa ziada.
Wakati mwingine, huenda wakahitaji kuwa kwenye kitengo cha utunzaji maalum kwenye
hospitali kwa muda mrefu na Upendo wa
Familia ni Nguzo ya Kwanza ya Mafanikio kwa mtoto huyu”.
Mama au wazazi wa mtoto njiti wanapokuwa
na upendo wa dhati na subira, wana uwezo wa kufanya maajabu. Mtoto njiti
anahitaji upendo mkubwa na uangalifu wa familia yake kwani upendo unaweza kuwa
nguvu ya kutia moyo katika kipindi kigumu. Kuwa karibu na mtoto wako, kumtunza,
na kumpa nafasi ya kujenga uhusiano wa karibu kunaweza kusaidia katika kupona
na maendeleo ya mtoto.
Naam, Makala hii leo inachungulia
dirisha la utoaji ruhusa ya likizo ya Uzazi kwa kina mama walio jifu ngua
watoto njiti. Pata utulivu wakutosha ilikusoma na kuelewa nyaraka zinasemaje,
wabunge wali wahi kuhoji nini juu ya Likizo ya Uzazi, wataalamu wa afya
wanashauri jambo gani kuhusu likizo ya uzazi kwa akina mama wanao jifungua
watoto njiti.
Tuanzie hapa kwenye Sheria ya Majadiliano ya
Utumishi wa Umma Na. 19 ya 2003, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya
2004 Na Sheria ya Asasi za Kazi Na. 7 ya 2004. Hata sharia hizi znyewe zilipo tungwa hazikuwajumuisha kina mama
wanaojifungua watoto njiti, zinasema mfanyakazi
anastahili likizo ya uzazi ya malipo ya siku themanini na nne (84) au siku mia
moja (100) iwapo atajifungua mtoto zaidi ya mmoja katika mzunguko wa miezi 36.
SWALI: Je,
wakati zinatungwa Sheria hizi hapakuwa na kina mama waliokuwa wakijifungua watoto
kabla ya muda wao (njiti), tena ambao ni watumishi wa umma?
“Mtoto
njiti, mara nyingi huwa na matatizo ya kiafya yanayohitaji uangalifu wa ziada.
Wakati mwingine, huenda wakahitaji kuwa kwenye kitengo cha utunzaji maalum
kwenye hospitali kwa muda mrefu. Mama na familia wanapokutana na hali hii,
wanajikuta katika hali ya kutatanisha, lakini ni muhimu kushirikiana na
wataalamu wa afya ili kutoa huduma bora kwa mtoto na kuwasaidia wazazi kuhimili
changamoto hizi” Huyo ni Dkt. Haika
Mariki kutoka Chama cha Madaktari bingwa wa watoto Tanzania (PAT).
JE, BUNGENI KUNAYAPI?
Mwaka
2019 Juni, Mbunge wa Viti Maalum, ANATROPIA THEONEST Aliwahi kuuliza swali bungeni….Je, ni likizo ya muda gani wamekuwa wakipewa wazazi (watumishi wanawake
na wanaume) pale wanapopata watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti?
2015-2020 |
Session 15 |
Sitting 52 |
Public Service Management |
Ofisi ya Rais (Menejimenti ya |
450 |
2019-06-25 |
Alie kuwa NAIBU WAZIRI, OFISI YA
RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA kwa wakati huo Dr.
Mary Machuche. Alijibu swali hilo
kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, “Kwa mujibu wa Kanuni H. 12(2) ya Kanuni za Kudumu
katika Utumishi wa Umma za Mwaka 2009, mtumishi wa umma mwanamke anapojifungua
mtoto hupewa likizo ya uzazi ya muda wa siku 84 mara moja kila baada ya miaka
mitatu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanuni H.
12(3) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009, mtumishi
husika anapojifungua watoto zaidi ya mmoja hupewa siku 14 zaidi za likizo ya
uzazi na hivyo kuweza kuwa siku 98. Kanuni tajwa haikubanisha muda wa likizo ya
uzazi kwa mtumishi anayejifungua mtoto njiti”.
Matukio ya uzazi wa mapacha zaidi ya wawili (triple) na watoto njiti ni nadra
kutokea mara kwa mara. Hivyo, Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka
2009 hazikuainisha masharti ya likizo ya uzazi kwa matukio kama hayo. Hivyo,
natoa wito kwa waajiiri na wasimamizi wa rasilimaliwatu katika utumishi wa umma
kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Utumishi na kuomba kibali cha kuongezewa muda
wa likizo ya uzazi kwa watumishi wa umma walio chini yao pindi wanapojifungua
watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti.
Kwa mujibu wa Kanuni H.13 ya Kanuni
za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009, Mtumishi wa Umma mwanaume
hupewa likizo ya uzazi ya angalau siku tano kuanzia siku ya kuzaliwa mtoto ili
aweze kuhudumia familia yake. Hata hivyo, iwapo kuna sababu za msingi
zinazomlazimisha kuendelea kuhudumia familia kwa ukaribu, mtumishi husika
anaweza kuomba ridhaa kwa mwajiri wake ya kuongezewa ili siku kadhaa kuhudumia
familia.
Inapotokea mtumishi wa umma kajifungua watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto
njiti na kulazimika kuwa na muda wa zaidi wa kuhudumia watoto hao, mwajiri wake
anapaswa kuwasilisha hoja kwa Katibu Mkuu (Utumishi) ilia toe kibali cha
kuongeza muda wa likizo ya uzazi.
Dkt. Haika Mariki anasema kutokana
nachangamoto wanazo zaliwanazo watoto hao ambao hawajatimiza mudawo wakuzaliwa,
kitaalamu tunaendelea kuishauri Serikali kupitia bunge waweze kupitisha sharia
itakayo walinda na kuwawezesha wamama wanao jifungua kabla ya wakati, na wakiwa
waajiliwa waweze kulea watoto wao kwa kipindi cha miezi 6 na kwa baba wa
mtoto njiti apewe likizo ya mwezi 1, ili aweze kumsaidia mwezi wake
kuhudumia mtoto wao.
Kwa mujibu wa
Taasisi ya Doris Mollel Foundation
inaonesha kwamba kuzaliwa kabla ya wakati ndio sababu kuu ya vifo vya watoto
wachanga walio chini ya umri wa miaka mitano, na kuchangia takriban 40%
ya vifo vya watoto wachanga. Ikizingatiwa kuwa kila mwaka watoto 336,000
wanaozaliwa kabla ya wakati huzaliwa nchini Tanzania, 11,500 hufariki
kutokana na matatizo ya kuzaliwa kabla ya wakati.
Ikumbukwe
kwamba Taasisi hii imekuw na mchango mkubwa katika kuwasaidia watoto
waliozaliwa kabla ya wakati pamoja na mama zao, ikiwemo kuwapatia vifaa muhimu
na mahitaji ya lazima baada ya kujifungua wawapo bado hospitali au waliopo
nyumbani.
Hata hivyo
Taasisi hiyo kwa kushirikiana wadau mbali mbali hivi karibuni wamekuwa
wakiiomba Serikali kufanyia marekebisho ya Sheria ya Likizo ya Uzazi hasa kina
mama wanao jifungua watoto kabla ya wakati (njiti), kuongezewa muda wa likizo
hiyo kufia miezi 6 na mwezi 1 kwa baba wa mtoto huyo, tofauti na
ilivyo sasa siku 84 kwa mama anae jifungua mtoto kabla ya wakati na siku
5 kwa baba mwenye mtoto. “Hadi sasa Serikali imetulia kama bahari
yenye kina kirefu” Nilini wataiona nuru wazazi wanaojifungua watoto wa aina
hii?.