Picha:un news.
Na, John Kabambala: Mara
nyingi, katika maisha yetu, tunakabiliana na ahadi zilizotolewa na watu wengine.
Ahadi hizi zina nguvu kubwa na zinaweza kujenga matumaini na furaha au kuvunja
mioyo na kusababisha uchungu hii inakuwa kwa watu wazima na Watoto pia
husisimka na kufurahi wanaposikia ahadi kutoka kwa wazazi wao, hata hivyo,
wakati mzazi anaposhindwa kutimiza ahadi hiyo, hisia za mtoto zinaweza
kujeruhiwa na kusababisha matokeo ambayo yanaweza kuathiri uhusiano wao na
mzazi wao.
Hisia za kuvunjika moyo, huzuni, na kutokuelewana zinaweza
kujitokeza, Mtoto anaweza kuanza kuhoji nia na upendo wa mzazi wake, wakati
mwingine huenda akaanza kuhisi kukosa thamani na kujiona kama mtu asiye na
umuhimu kwenye familia yao.
Uhusiano kati ya mzazi na mtoto unaweza kuathirika sana kwa
sababu ya ahadi iliyovunjwa. Ikiwa mtoto hajashughulikiwa ipasavyo na mzazi
wake, huenda akawa na hasira, kukasirika, au hata kujitenga. Hisia hizo
zisizoeleweka na kutokuelewana zinaweza kujenga ukuta kati ya mzazi na mtoto,
na hivyo kudhoofisha uhusiano wao wa karibu, Makala hii inaangazia athari za ahadi za
Wazazi zisizotimizwa kwa watoto wao:
CHANZO CHA TATIZO:
Likizo ya wanafunzi ni kipindi muhimu ambacho watoto hupata
muda wa kupumzika na kufurahia shughuli zisizo za kimasomo. Hata hivyo, baada
ya likizo kumalizika, ni muhimu kwa wazazi kuzingatia mambo kadhaa ili
kuwawezesha watoto wao kurejea katika utaratibu wa shule kwa ufanisi.
Kumalizika kwa likizo ya wanafunzi ni tukio ambalo hutangaza
mwisho wa kipindi cha mapumziko na kurejea kwa shughuli za kawaida za masomo.
Likizo hii mara nyingi inajumuisha muda wa miezi kadhaa, ambapo watoto
hujihusisha na shughuli za burudani, mapumziko, na kujenga uhusiano na familia
zao.
Hata hivyo, baada ya
likizo kumalizika, ni muhimu kwa wazazi kuchukua hatua muhimu ili kuwasaidia
watoto wao kurejea katika mazingira ya shule na kujitayarisha kwa masomo
yanayofuata, Ilikupata maelezo na ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu ahadi wanazo
toa wazazi kwa watoto wao juu ya ununuzi wa vitu vipya nimemtafuta
Mwanasaikolojia na Dkt. Wa mama na mtoto kutoka Morogoro, Dkt.Magdalena Kongera.
Picha ya Dkt.Magdalena Kongera.
SWALI: Wazazi
wanapaswa Kufanya na Kuepuka nini wakati wa likizo ya
wanafunzi inapo malizika?
Dkt.Magdalena Kongera
: “Wakati likizo ya wanafunzi
inapokaribia kumalizika na Shule zinapo funguliwa, wazazi wanapaswa kuwa wawazi
kwa watoto wao kwanza kuwazoesha watoto wao kuwambia kama nitapata pesa
nitakunulia begi jipya, nguo mpya na viatu vipya maneno haya huwakaa zaidi
watoto. Mzazi hapaswi kumuonesha mtoto kila sikukuu anunue kitu kipya, maana
yake siku ambayo hatapewa kitu kipya kuna mambo mawili moja mtoto anaweza
kuathirika kisaikolojia au kujitoa uhai wake”.
SOMA KISA HIKI KUTOKA
MOROGORO KWA MWALIMU MATHIAS KITONTO:
Mathias Kitonto: Ni
Mwalimu alie hitimu miaka mitatu iliopita katika chuo kimoja kilichopo Mkoani Morogoro, nimemtafuta ili
kunielezea kisa cha mtoto Ally Juma, kisa hicho amewahi kukifahamu kutoka kwa
mtoto huyo akiwa Shuleni, jinsi “ahadi ambayo wazazi walishindwa kuitimiza ilivyo
athiri maisha ya mtoto huyo” .Mwalimu huyu ameomba kutotumia jina lake
halisi pamoja na mtoto huyo kwani kisa hiki kinaihusu familia ya karibu nae.
SWALI: Mwalimu ! Unafahamu nini kuhusu kisa cha wazazi walioshindwa kumtimizia
ahadi mtoto wao?
”Nakumbuka kulikuwa na
familia moja Wakati wa likizo, baba na
mama walikuwa na mazungumzo mengi kuhusu jinsi kumpa mtoto wao uzoefu wa kipekee, hususani
kumpeleka maeneo ambayo hajawahi kuyafika nan i nadra sana kufika.
Kwa miezi kadhaa,
familia hiyo ilipanga safari ya kuvutia kwenda Hifadhi ya Mikumi inayojulikana
kwa mandhari yake ya ajabu na wanyama porini mbalimbali. Hata hivyo, siku ya
kurudi shuleni ilipofika, wazazi hao wawili walikuwa na msongo wa mawazo. Jioni
kabla ya kurudi kijijini, walifanya uamuzi ulioathiri maisha ya mtoto wao, Waliamua
kufuta safari hiyo ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Baada ya kuwasili nyumbani,
Ally Juma alitarajia kusikia habari
njema za safari hiyo. Lakini badala yake, alikaribishwa na habari ya kuvunjiwa
ahadi. Alibaki ameduwaa na kuchanganyikiwa. Wazazi wake walijaribu kumfariji,
wakisema kwamba safari hiyo ingefanyika wakati mwingine, lakini uaminifu na
imani ya Ally Juma kwa wazazi wake
vilipungua”.
SWALI: Kuna madhara yeyote ali aliyapata kutokana na kushindwa
kutimiziwa ahadi?
Mwl. Mathias Kitonto: “Ndiyo,
madhara ya ahadi za wazazi wakati wa
likizo hayakuishia tu kwa hisia za mtoto, yalikuwa na athari kubwa katika
maendeleo yake ya kihisia na kiakili, Kwanza, Mtoto huyo alianza kupoteza
imani katika ahadi zilizo kuwa zikitolewa na wazazi wake na alianza kuwa na
uoga wa kujenga matarajio yoyote dhidi yao. Hii ilikuwa na athari mbaya kwa
uhusiano wake na watu wengine, kwani alikuwa na wakati mgumu kuamini na
kuwategemea wengine.
Pili, mtazamo wake
kuelekea wazazi wake ulibadilika. Alianza kuhisi kukosa uaminifu na kujitenga
nao. Alikuwa na hisia za kujisikia peke yake na kutokuwa na thamani. Hii
ilikuwa hatari kwa uhusiano wao, kwani Ali alianza kupunguza mawasiliano yake
na wazazi wake na kuweka ukuta kati yao.
Zaidi ya hayo, Ally alianza kukosa hamu na motisha ya
kujaribu vitu vipya, Ahadi ya safari ya
kusisimua ilikuwa imechochea hamu yake ya kujifunza na kugundua mambo mapya lakini
sasa, hamu hiyo ilizimwa alianza kukata tama, Madhara haya yalitanda kama wingu
jeusi juu ya maisha ya mtoto huyo hapo
awali alikuwa mvumilivu na mwenye furaha, lakini sasa amekuwa mtu mwenye
wasiwasi na aliyejaa hofu, Uwezo wake wa kustawi katika shule umepungua, na
urafiki wake na watoto wengine ulidhoofika”. Alisema Mathias Kitonto.
ATHARI ZA AHADI ZA WAZAZI ZISIZO
TIMIZWA KWA WATOTO:
Ikumbukwe kwamba mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu kijiji cha Ikengwa
Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma mtoto wa darasa la nnealijinyonga kwa sababu ya
wazazi wake kushindwa kumnunulia nguo za sikukuu ya EID, lakini pia katika
Manispaa ya Morogoro mtoto mwenye umri wa miaka tisa (9) alijinyonga kwa sababu
ya wazazi wake kushindwa kutimiza ahadi kwa mtoto wao.
MAMBO YA
KUEPUKA: “Wazazi hawapaswi kuwaahidi watoto wao kila likizo au sikukuu
kwamba wanunue zawadi au kuwapikia chakula tofauti nakile kilichozoeleka
kupikwa nyumbani kilasiku,hata kama uwezekano huo upo wa kutimiza hayo yote
wakati mwingine wazazi wanashauriwa wasifanye chochote kipya ilikuwazoesha
watoto utofauti wa hali ya maisha ya kila
siku.
Kwa kufanya hivyo watoto watazoea
kwamba hata sikuku nyumbani mama anaweza kupika chakula chochote na siolazima
kwamba kipikwe chakula kipya, hata likizo ikiisha watoto wanweza kuendelea na
yunifomu zilezile za tangu likizo ilioisha, sio kila likizo ununue kvipya
vyote”. Dkt.Magdalena Kongera, alisema.
Baada ya likizo ya wanafunzi kumalizika, ni jukumu letu kama
wazazi kuzingatia mambo muhimu ili kuwasaidia watoto wetu kurejea katika
utaratibu wa shule kwa ufanisi. Kwa kuweka ratiba thabiti, kusaidia kazi za
shule, kukuza ustadi wa kusoma na kuandika, kushiriki katika shughuli za
kimwili, na kujenga mawasiliano mazuri na watoto wetu, tunaweza kuwahakikishia
mafanikio yao ya kitaaluma na ustawi wao kwa ujumla. Juhudi zetu kama wazazi
zinaweza kuchangia sana katika kujenga msingi imara kwa watoto wetu na
kuwawezesha kuwa viongozi wa baadaye wenye mafanikio.