Picha ya Vailet Bukuku:
Na, John Kabambala: Mkoa wa Mbeya, upo nyanda za juu kusini na mpakani kabisa mwa
Tanzania na Zambia, ni eneo lenye uzuri wa asili, utajiri wa tamaduni, na
historia ndefu na yapekee katika taifa hilo tulivu la Tanzania. Hata hivyo, mkoa
huo pia unakabiliwa na changamoto kubwa ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU),
ambayo yanawaathiri zaidi vijana balehe. Boda ya Tunduma nikati ya njia kuu
zinazo tumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kuelekea mataifa jirani ya Afrika
Kusini, Zambia,DRC, Rwanda na mengineyo. Ili kuelewa vyema jinsi tatizo hili lilivyo
kiasi cha kuathiri jamii na jinsi linavyoweza kushughulikiwa, fuatilia makala
hii inayo angazia historia ya VVU tatizo, chanzo na suluhisho lake mkoani humo.
HALI ILIVYO KUWA:
Ilikuwa ni miaka
ya 1980 na 1990 ilishuhudia janga la maambukizi ya VVU lilipo anza kuenea kwa
kasi zaidi ulimwenguni pote, na Tanzania haikuwa tofauti na mataifa mengine, Giza
nene likaanza kuwaandama vijana balehe na watu wazima wa Mkoa wa Mbeya kwa
kimya kimya. Ambapo mlipuko wa maambukizi ya VVU, yaani virusi vinavyosababisha Ukimwi, ulikuwa unapata nguvu
kwa kasi zaidi na Vijana wakawa ndio waathirika wakubwa wa janga hilo, mkoa huo
ukawa kwenye hatari zaidi kutokana na mwingiliano wa watu wa nchi jirani
kupitia boda ya Tunduma.
Kwa mujibu
wa Takwimu za Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) za mwaka 2020, zinaonesha kwamba Mkoa wa Mbeya upokwenye
nafasi ya tatu kwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya UKIMWI hasa kwa vijana
walio kati ya umri wa rika balehe kwa asilimia 9.3%, Mkoa wa Njombe ukiwa nafasi ya kwanza kwa kuwa na maambukizi
ya asilimia 11.4% ukifuatiwa na Mkoa
wa Iringa kwa kuwa na maambukizi ya asimia 11.3%,
CHANZO CHA MAAMBUKIZI KWA VAILETH BUKUKU:
Wazazi walitengana, Umasikini wa kipato ndani ya familia, Kubakwa, Uhaba wa elimu na uelewa juu ya VVU na njia za maambukizi, Elimu sahihi shuleni
au nyumbani juu ya ngono salama na Afya ya Uzazi, hivi ni miongoni mwa vyanzo
vya maambukizi ya VVU.
Kufikia miaka
ya 2015 hivi, kijana mmoja jasiri aliekuwa shujaa asiyejulikana kwa hali yake kwa
shauku kubwa akaanza kutamani kueneza mwanga wa maarifa kuhusu VVU katika jamii
ya vijana wa Mbeya. Alijua kuwa angejitokeza wazi kuzungumzia jambo hilo
ilikuwa njia nzuri ya kuwasilisha ujumbe unaoweza kugusa mioyo na kubadilisha
mitazamo zaidi kwa vijana wa mkoa huo. Hivyo basi, akaamua kuanza safari yake
ya kuwaelimisha vijana kuhusu maambukizi ya VVU kupitia historia yenye kuvutia na
ya ukweli katika maisha yake, japo ilikuwa ngumu saana kwake na kuaminika kwa
vijana wenzake.
Makala hii
imejikita zaidi kufahamu mwenendo wa maisha ya kijana huyo jasiri na shujaa
aitwae Vaileth Bukuku tunae mzungumzia leo, tangu
alipo tambua hali yake ya maambukizi akiwa na umri wa miaka nane (8) hadi leo
hii, mchango wake ni upi kwa jamii inayo mzunguka kuhusu elimu anayo itoa kwa vijana
kuhusu VVU.
SWALI: Vaileth! Unakumbuka nini kabla hujatambua
hali yako kiafya?
Vaileth Bukuku: “Nakumbuka nikiwa na umri wa miaka nane tu (8) majira ya saa moja usiku hivi nikiwa
nyumbani kwetu kijana mmoja nilie mfahamu kama rafiki wa dada yangu
alibadilisha historia ya maisha yangu, kutoka kwenye historia yenye furaha hadi
kuwa kumbukumbu yenye uchungu, sitasahau. Nakumbuka ilikuwa sikukuu ya pasaka dada yangu aliniacha nyumbani
nikiwa na njaa akaenda disko jioni yapata kama saa moja hivi, alikuja kaka
mmoja nyumbani ambae alikuwa na mazoea na dada yangu alipofika akaniuliza
Vaileth umekula? Nikamwambia hapana sijala akaniambia njoo uchukue pesa ukanunu
mchele uje upike, akanipatia shiringi elfu moja nikaenda dukani kununua mchele.
Badae alirudi tena
huyo kaka! Akaniuliza unatamani kunywa soda? Nikamjibu
ndio natamani akaniambia twende dukani ukachukue soda, yule kaka hakunipeleka
dukani akanipeleka chooni tulipofika chooni akaniambia nivue nguo nikakataa
akanilazimisha nakuniambia ukipiga kelele nitakuua, akaniziba mdomo kwa wake
wakushoto akanivua ngua kwa lazima, nakunibaka baada ya kumaliza kitendo kile
akakimbia niliumia sana baadae nikajivuta kutoka chooni kuelekea ndani, nilishindwa
hata kuingia ndani ya nyumba nika lala mlangoni, dada aliporudi usiku sana
akanikuta mlangoni akanibeba hadi ndani”.
SWALI: Dada
yako alipo kufikisha ndani alitaka kufahamu nini kutoka kwako?
Vaileth Bukuku: “Kwanza
alitaka kufahamu kipi kimesababisha hadi damu zitoke kiasi hiki, nikamuelezea kwamba
rafiki yako wakiume ambae hua anakuja hapa nyumbani alikuja jioni muda mfupi tu baada yaw ewe
kwenda disiko alipofika aliniuliza kama nimekula au la! nikamjibu hapana
sijala, akanipatia pesa yakwenda kununua kilomoja ya mchele, nilipo rudi kutoka
dukani akajatena akaniuliza unatamani kunywa soda nikajibu ndio akaniambia
twende dukani nikakununulie, hakunipeleka dukani badala yake akanipeleka chooni
kufika huko ndio kanibaka”.
SWALI: Baada ya
kumuelezea dada yako tukuio lilivyo tokea alifanya nini usiku ule?
Vaileth
Bukuku: “Dada alisema nisinge ondoka yawezekana usinge fanyiwa kitendo hiki”, “kisha
akachemsha maji yamoto akanikanda
akanipatia na panado akanimbia usimwambie mtu yeyote, hili nijambo la aibu sana”.
SWALI: Baada ya
kipindi gani ulianza kuona mabadiliko ya kiafya kwenye mwili wako?
Vaileth Bukuku: “Baada ya miezi mitatu nilianza kuumwa mara
kwa mara vidonda vikaanza kumtoka nikashindwa hata kuudhulia masomo shuleni,
siku moja alikuja jirani yetu nyumbani
akaniuliza mbona sikuhizi hujikucheza na watoto wenzako nyumbani na sikia hata
shuleni huendi unatatizo gani? Aliuliza lakini sikumwambia, kesho yake akarudi
tena ikabidi nimwambie ukweli kuwa mimi nina umwa akanichukuwa akanipeleka
hospitali tulipofika daktari akamwambia yule mama nenda polisi ukachukue pf3
maana anaonekena huyu binti kunakitendo alifanyiwa mbali na magonjwa ya zinaa
anamaambukizi ya virusi vya ukimwi ”.
Mnamo mwaka 2016
katika halmashauri ya jiji la Mbeya kupitia Shirika la Tumaini Community Services lenye makao
yake makuu Mkoani huo baada ya kuona ongezeko la maambuki ya virusi vya UKIMWI
kwa vijana balehe yanashamiri, walianzisha mradi wakuwawezesha vijana kupata
elimu ya afya ya uzazi, elimu ya upimaji wa vvu, elimu ya kujitambua na elimu
ya uchumi. Na hapa ndipo Vaileth alipo kutana na Shirika hili kupitia
mradi wa ujulikanao kwa jina la Dreams yaani (Ndoto).
Kupitia mradi huo unaotekelezwa Mkoani Mbeya kwa halmashauri
tatu ambazo ni Mbeya mjini, Kyela na Mbarali kwa ufadhili
wa mfuko wa Rais wa Marekani wa harakati za kupambana na UKIMWI, yaani (PEPFAR)
kanda ya Tanzania, ambao unalenga kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa
vijana kwa kuwapatia elimu ya kujikinga na maambukizi ya vvu, elimu ya
kujitambua, na elimu ya kiuchumi.
Wataalamu
kutoka shirika hilo walimshauri binti
huyo kuwa mfusi mzuri wa matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi na
kuendelea kujilinda yeye mwenyewe na kuwalinda wengine ilikutoendelea kuchochea
maambukizi mapya kwa jamii, hasa kwa vijana balehe.
SWALI: Ulikuwa na ndoto gani maishani?
Vaileth Bukuku: Ndoto zake zilikuwa
za kusoma na kuwa muhandisi wa kompyuta, japo hakuifikia ndoto hiyo lakini anashukuru
mradi wa Dreams kupitia shirika la Tumaini
Community Services baada ya kumfikia walimpeleka chuo cha ufundi VETA kujifunza ufundi wa kushona na
kompyuta ambapo baada ya kuhitimu walimkabidhi vyeleani na vifaa vingine vya
kufanyia kazi, pamoja na mabinti wezake anao wasimamia kwenye kikundi, na sasa
wamejiajili wenyewe wanajipatia kipato, na wakiendeleza elimu kwa vijana kuhusu
kujikinga na maambukizi ya VVU.
SULUHISHO LA
MAAMBUKIZI YA VVU?
Ushauri
wake kwa vijana ambao tiyari wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi Vaileth anasema, wafuate ushauri wa wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia muda wa matumizi
sahihin ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi, wajilinde na wawalinde wengine
wasisambaze virusi vya Ukimwi kwa makusudi kwa wale ambao hawajapima kujua hali
zao za kiafya wajitokeze wakapime kujua hali zao ilikuishi kwa Amani na furaha,
ilikama hawana maambukizi waendelee kuwa waamifu na wale ambao watagundulika
kuwa na maambukizi ya vvu waanze kliniki mapema.
“Mimi tangu
nijue hali yangu ya afya nina amani, furaha na nimfuasi mzuri wa dawa na
mwaminifu kwa wengine” Alisema Vaileth Bukuku.