By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: Hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano-Morogoro
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Uncategorized > Hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano-Morogoro
Uncategorized

Hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano-Morogoro

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/04 at 8:18 AM
By Tanzania Kids Time 9 Min Read
Share
SHARE


Hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka
mitano-Morogoro
Utapiamlo ni hali ya upungufu wa lishe au lishe
iliyozidi. Tunapozungumzia upungufu hapa tunazungumzia udumavu ambao ni
utapiamlo wa muda mrefu (chronic malnutrition), ukondefu ambao ni utapiamlo wa dharura
(Acute Malnutriton) na uzito pungufu (Underweight) ambao huonekana kwa watoto
wenye udumavu na ukondefu. Vile vile utapiamlo unaweza kuwa wa upungufu wa
virutubishi muhimu vya vitamini na madini ambavyo pamoja na kwamba mahitaji
yake ni kidogo lakini umuhimu wake ni mkubwa sana kwa afya na Ustawi wa
binadamu. Upungufu wa vitamin na madini unajulikana pia kama utapiamlo
uliojificha au (hidden hunger) kwa kuwa madhara yake hayaonekani mapema. Aina
nyingine ya utapiamlo ni ule wa lishe iliyozidi ambayo inapelekea magonjwa sugu
yasiyoambukizwa yatokanayo na chakula, kama kisukari, magonjwa ya moyo,
shinikizo la damu na hata baadhi ya kansa.
Sababu ya kuwepo
kwa utapiamlo zimegawanyika katika makundi matatu:
1.     
Sababu za karibu
(immediate causes)
                                
i.           
Ulaji duni na
                              
ii.           
Magonjwa
2.     
Sababu zilizojificha
(undelying causes) hizi ni zile sababu zinazopelekea uwepo wa sababu za karibu
ambazo ni:
                                
i.           
Upungufu wa uhakika
wa chakula katika kaya,
                              
ii.           
Upungufu katika matunzo
ya makundi maalumu ya watu, na
                            
iii.           
Upungufu katika huduma
za msingi za afya katika jamii
3.     
Sababu za Msingi
(Basic causes) hizi ni zile sababu zinazopelekea kuwepo kwa sababu wezeshi na
sababu za karibu:
                                
i.           
Elimu duni
                              
ii.           
Rasilimali
a.      
Udhibiti wa
rasilimali watu, uchumi na rasilimali za mashirika
b.     
Mfumo wa siasa na
itikadi, Mfumo wa uchumi, mila na desturi
Sekta mtambuka
zinahusika na kuzuia utapiamlo ni sekta za kilimo na uhakika wa chakula, Afya
na Ukimwi, Maji, mazingira na usafi, Elimu, Maendeleo ya mtoto, usalama katika
Jamii, Mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, Mipango, Maendeleo ya Jamii na
Jamii kwa ujumla
Jinsi ya kuzuia
utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano:
Jambo hili linatakiwa kuanza hata kabla wanawake
hawajawa wajawazito. Hivyo ni muhimu kusimamia hali ya lishe ya wanawake katika
umri wa kuzaa ili watakapokuwa wajawazito wawezeshe kukuwa vyema kwa kiumbe
kinachokuja. Siku 1000 ni za Msingi sana katika kuzuia utapiamlo kwa watoto.
Siku 1000 zinajumuisha siku 270 za ujauzito, siku 730 za mtoto katika miaka
miwili ya mwanzo. Udumavu unaotokea na kutorekebishwa katika siku 1000 za
kwanza hautaweza kurekebishwa tena.
Kuzuia utapiamlo:
Afua zinazolenga kupunguza/kuzuia udumavu na
utapiamlo ni zile zinazolenga siku 1000 ambazo ni kuanzia mama anapokuwa
mjamzito hadi mtoto anapofikia umri wa miaka miwili.
i.              
Kuboresha lishe ya
Jamii yaani watoto wadogo na wachanga, vijana, wanawake na wanaume
ii. Mama kuhudhuria kliniki mara anapojihisi mjamzito
iii.          
Mjamzito kupata dawa
za kuongeza damu madini chuma na aside ya foliki
                            
iii.           
Mjamzito kupata dawa za
kutibu malaria na minyoo
                            
iv.           
Mwenza na Mjamzito
kupata ushauri wa lishe, kupumzika wakati wa ujauzito na maandalizi ya Uzazi
                              
v.           
Matibabu ya magonjwa
wakati wa ujauzito
                            
vi.           
 Mama mzazi kupata dawa za kuongeza damu na
nyongeza ya vitamin A katika siku 42 baada ya Uzazi
                          
vii.           
Mama mzazi
anashauriwa kupata Huduma za Uzazi wa mpango ili awe na muda wa kulea mtoto na
familia
                        
viii.           
Mama mzazi
anashauriwa lishe yake mwenyewe wakati wa ujauzito na anaponyonyesha
                            
ix.           
Mama anashauriwa
kunyonyesha mtoto maziwa ya mama tuu mara anapozaliwa kwa muda wa miezi sita ya
mwanzo
                              
x.           
Mtoto aanzishiwe
vyakula vya nyongeza mara anapofikia umri wa miezi sita huku akiendelea
kunyonyeshwa maziwa ya mama hadi atakapofikia umri wa miaka miwili au zaidi
                            
xi.           
Mama kumpeleka mtoto kliniki
kwa ajili ya Huduma za chanjo ili kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa chanjo
                          
xii.           
Ushauri unatolewa wa
njia za kupata chakula kutoka makundi mbalimbali kwa kulima mbogamboga na
kufuga wanyama wadogo
                        
xiii.           
Ushauri wa usafi wa
mazingira, vibuyu chirizi na matumizi ya vyoo bora na kanuni za usafi
zinatakiwa kuzingatiwa ili kuzuia magonjwa yanayoweza kupelekea utapiamlo kwa
kuwa wakati wa ugonjwa watoto hukosa hamu ya kula hivyo kupelekea kupungua
uzito na wanapopungua uzito hali zao za kinga hupungua hivyo kupelekea watoto
kupata magonjwa ya mara kwa mara na mwisho hufikia hali ya utapiamlo
                        
xiv.           
Mikakati ya kupunguza
utapiamlo yanatakiwa kufanyika katika sekta mtambuka za kilimo na uhakika wa
chakula, afya na UKIMWI, maji na usafi wa mazingira (WASH), Elimu, usalama
katika Jamii (Social protection), mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na
katika Ngazi ya Jamii kwa ujumla
                          
xv.           
Afua nyingine za
kupunguza utapiamlo ni pamoja na urutubishaji wa vyakula kama vile nafaka kama
unga wa ngano na mahindi zinaongezwa madini ya zinki na madini chuma, vilevile
asidi ya folik na vitamini B 12. Mafuta ya kula huongezwa vitamin A na chumvi
huongewa madini joto.
                        
xvi.           
Watoto hupatiwa
nyongeza ya vitamin A na dawa za kutibu minyoo kila mwezi wa sita na wa kumi na
mbili; Huduma hii hutolewa sambamba na kupima hali ya lishe na kisha kupatiwa
matibabu kwa wenye utapiamlo mkali
Hali ya lishe
kwa Mkoa Morogoro
Hali ya udumavu katika mkoa Morogoro umepungua
kutoka asilimia 44.4 (TDHS, 2010), asilimia 36.9 (NNS, 2014) na kufikia
asilimia 33.4 (TDHS, 2015-2016). Malengo ya kitaifa ni kufikia asilimia 28
ifikapo mwaka 2021.
Hali ya ukondefu (utapiamlo wa dharura) ilikuwa
asilimia 5 (TDHS, 2010) na kuongezeka mpaka asilimia 6 (TDHS, 2015-2016)
malengo ni kufikia asilimia chini ya 5 mwaka 2021.
Upungufu wa damu kwa wanawake katika umri wa kuzaa
ilikuwa asilimia 45 (TDHS, 2010) na imeongezeka kufikia asilimia 47.5 (TDHS,
2015-2016), kiwango hiki kinatakiwa kufikia asilimia 33 ifikapo mwaka 2021.
Upungufu wa damu kwa watoto chini ya miaka mitano
imeongezeka kutoka asilimia 59 (TDHS, 2010) hadi kufikia asilimia 65.7 kwa
(TDHS, 2015-2016).
Utekelezaji wa afua za lishe Tanzania unafuata
mpango mkakati mtambuka wa lishe wa Taifa wa mwaka 2016-2021unaolenga watoto,
vijana wanawake na wanaume wa Tanzania wawe na lishe bora itakayopelekea maisha
na afya bora ambayo yataongeza uzalishaji na kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja
na wa taifa hivyo kufikia Maendeleo endelevu.
Maeneo saba ya kipaumbele ya Mkakati mtambuka wa
lishe wa Taifa (2016-2021) ni:
·        
Kuinua lishe ya
wanawake katika umri wa kuzaa, watoto wachanga na wadogo na vijana
·        
Kuinua mikakati ya
kuzuia na kutibu upungufu wa vitamin na madini
·        
Kuinua mikakati ya
matibabu jumuishi ya utapiamlo wa dharura (ukondefu)
·        
Kuzuia na kutibu
magonjwa sugu yasiyoambukiza yatokanayo na chakula
·        
Kuinua mikakati
jumuishi ya lishe katika sekta mtabuka ambazo ni kilimo na uhakika wa chakula,
afya na UKIMWI, maji na usafi wa mazingira (WASH), Elimu, usalama katika Jamii
(Social protection), mazingira na mabadiliko ya tabia nchi
·        
Kuimarisha mikakati
ya lishe na utawala katika sekta mtambuka
·        
Kuanzisha Uratibu wa
takwimu za masuala ya lishe katika sekta mtambuka
Je lishe ni
nini?
Lishe ni mchakato unaohusika tangu chakula
kinapoliwa, kumengenywa na kuchukuliwa na seli za mwili kwa ajili ya matumizi
katika mwili.
Makundi ya vyakula ambavyo vinashauriwa:
  1. Nafaka mizizi na ndizi mbichi
  2. Jamii ya mikunde na vyakula vitokanavyo na
    wanyama
  3. Mboga mboga
  4. Matunda
  5. Mafuta na sukari kwa kiasi
Bila kusahau maji ya kunywa safi na salama.

You Might Also Like

ENERGY AND NEO-COLONIALISM IN AFRICA, NO ANSWERS?

WAHITIMU WATAKAO JIUNGA DARASA LA KWANZA MWAKA 2023

ATHARI ZA NDOA ZA UTOTONI KIUCHUMI

SIKU YA WATOTO WALIOZALIWA KABLA YA KUKOMAA

ATHARI ZA NDOA ZA UTOTONI KIELIMU

Tanzania Kids Time February 11, 2018
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article je unafahamu mahusiano ya ngozi kati ya mama na mtoto wake?.
Next Article Watoto walio achiliwa hulu SUDANI KUSINI kutoka kwenye vikosi vya wapiganaji sasa wafundishwa ujasiriamali.
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?