Tarehe
13 mwezi Februari ni siku ya redio duniani, ambapo mwaka huu inafanyika
wakati matangazo ya Redio ya Umoja wa Mataifa yakitimiza miaka 69.
Katika ujumbe wake kwa mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni, UNESCO, likitoa wito wa kushirikisha zaidi
vijana katika vyombo vya habari.Mkurugenzi mtendaji wa UNESCO Irina
Bokova amesema mara nyingi vijana wa kike na wa kiume wenye umri wa
chini ya miaka 30 wanatengwa katika kuandaa na kutangaza vipindi vya
radio, na kwa mantiki hiyo, amevisihi vyombo vya habari na hasa redio
kuwapa vijana nafasi ya kujieleza.
Nchini Tanzania hilo limeanza kutendeka na mtandao wa wanahabari
watoto, ambao, kupitia usaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia watoto, UNICEF , unahamasisha watoto kujifunza utalaam wa
kutengeneza taarifa na vipindi mbalimbali za redio, na hivyo kupata
nafasi ya kuzungumzia kinachowagusa zaidi.
Ni namna gani redio imewawezesha katika maisha yao? Tuungane na watoto hao Tanzania