IFAKARA FEBRUARY 14, 2018
Martini Center ni Kituo cha masomo ya ziada kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro kimewaomba wazazi, walezi wasiwache watoto nyumbani mara baada ya kutoka shuleni ni vyema kuwapeleka katika vituo vya masoma ya ziada ili watoto wapate muda mrefu wakusoma lengo likiwa ni kufaulu kwakiwango kinacho takiwa kwenye masomo yao.
Akizungumza na Tanzania Kidistime Mwalimu Martini amesema hayo baada ya kuona baadhi ya wazazi kuwaacha watoto wanapotoka shule bila kuwatafutia masoma ya ziada ambayo husaidia mwanafunzi kuongeza molali na mazingatio ya masoma pamoja na kupata hali ya kujiamini wakati wote.
Aidha Martini amesema mwanafunzi hmijengea hali nzuri ya kiafya , akili na kuwa na msukumo wa kusoma kila siku hali ambayo huweza kumuongezea mtoto uelewa zaidi wa masomo yake.
Hata hivyo Mwalimu Olesti Asenga wa Martini Center amewaomba walimu wenzake wafundishe wanafunzi kwa maadili mema na kufuata mitaala iliyopo na ni bora kutafuta maarifa zaidi juu ya ufundishaji wa watoto wanapopata muda wa masomo hayo wazingatie masomo yao wakati wote kwani elimu ndio msaada wa maisha yao.
Wazazi na Walezi Mji mdogo wa Ifakara mkoani morogoro wameshauliwa kuwapeleka Watoto waokwenye masomo ya ziada baada ya kutoka shuleni ilikuwasaidia ufahamu wao.
Leave a comment