Ukuaji wa ubongo wa mtoto unaanza tangu mimba inapotunga. Imedhihirika
kitaalamu kuwa ubongo wa mtoto hukua kwa kiwango cha 80% katika kipindi cha
ujauzito hadi miaka 3 ya mwanzo ya maisha yake. Kuna uhusiano mkubwa kati ya
afya ya mjamzito na ukuaji wa ubongo na akili ya mtoto. Maendeleo ya ubongo wa
watoto yapo mikononi mwa wazazi ingawa majirani na ndugu wengine huchangia sana
katika maendeleo ya ubongo wa mtoto.