Kutoka Uganda shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,
UNHCR limesema mmiminiko wa wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya
Kidemokrasai ya Kongo (DRC), siku hizi umekuwa kinyume kabisa na matarajio ,
mwaka huu wakimbizi 60,000 wameingia, na kuibua changamoto katika utoaji wa
misaada ya kibinadamu kwao.
Joyce Munyao-Mbithi Afisa Mwandamizi wa Uhusiano wa UNHCR, Uganda amesema
kwamba katika siku chache zilizopita, wameanza kupokea wakimbizi Zaidi ya 1,000
kwa siku wakiwa wameangezeka kutoka wakimbizi kati ya 200 na 300 mapema wiki
iliopita.
Amefichua kwamba wamepokea takriban elfu tano kabla ya kumaliza hata miezi
mitatu ya mwaka huu ambamo walitarajia wakimbizi wasiozidi elfu sitini.
Hata hivyo ameongeza kuwa
wanakabiliwa na changamto za kuwahudumia na kwamba watakabiliwa na kipindi
kigumu zadi endapo wahisani hawatajitolea kutoa misaada Zaidi.
Mgogoro wa kikabila Jimboni Ituri na mashambulizi ya vikundi vilivyojihami
katika Jimbo la Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndio sababu
ya mmiminiko huu wa wakimbizi
Aidha Munayo-mbithi amesema haya wakati UNHCR, na wadau wake wanakumbana na
mlipuko wa maradhi ya kipindupindu ambayo kwa sasa yameambukiza wakimbizi Zaidi
ya 1,000 wakiwemo 33 waliothibitishwa kufariki dunia. Taarifa hii ni kwa hisani ya news.un.org/sw