Shirika la afya duniani, WHO linasema kila mzazi anakuwa na uchungu tofauti
wakati anakaribia kujifungua hivyo watoa huduma wahakikishe kuwa huduma hizo
zinazingatia mahitaji ya kila mtu badala ya kutumia aina moja ya huduma kwa
watu wote.
Tunahitaji wanawake wajifungue
katika mazingira salama, wakisaidiwa na wauguzi wenye ujuzi katika vituo vya
afya vilivyo na vifaa vyote vinavyohitajika
Hayo yamesemwa na shirika la afya
ulimwenguni WHO katika muongozo mpya lililoutoa wa mapendekezo ya kuanzisha
viwango vya kimataifa vya huduma kwa kina mama wajawazito wasio na matatizo
yoyote na kupunguza kuwapa usiyohitajika wakati wa kujifungua.
Hata hivyo Dkt. Princess Nothemba Simelela mkurugenzi msaidizi wa WHO
kwa masuala ya familia, wanawake, watoto na barubaru amesema ongezeko la
matumizi ya madawa katika mchakato wa kujifungua kawaida , linaathiti uwezo wa
mwanamke wa kujifungua na pia uzoefu wake katika kitendo hicho.
“Endapo uchungu unaendelea kawaida na mama na mwanae wako katika hali
nzuri , hawahitaji kupata usaidizi wa dawa za kuongeza kasi ya uchungu.”
Muongozo huo mpya wa WHO unatambua kwamba kila uchungu na kila kitendo cha
kujifungua ni tofauti kwa kila mama, hivyo katika kupunguza usaidizi wa dawa
kwa kina mama wakati wa kujifungua , muda unaotumika wakati mama akiwa katika
uchungu hadi wakati anapojifungua usitumike kama kigezo cha kumpa mama dawa za
kuongeza kasi ya uchungu au kutaka kumzalisha mapema.
Pia muongozo unasemna kina mama wengi wanataka kujifungua kawaida na
wanapendelea kutumia uwezo wa mwili wao kujifungua badala ya kupewa usaidizi wa
dawa.
Duniani kote inakadiriwa kuna matukio milioni 140 ya kujifungua kila mwaka na
asilimia kubwa hufanyika bila matatizo yoyote kwa kina mama na watoto. Lakini
katika miaka 20 iliyopita wauguzi wameongeza matumizi ya madawa ambayo siku za
nyuma yalitumika tuu kuepusha hatari au kuzuia matatizo kwa mtoto au mama
na hivyo kuongeza kasi ya uchungu au kufanya upasuaji.
Kwasasa WHO inataka madaktari na
wauguzi kuwashauri kina mama wajawazito wasio na matatizo kuwa muda wa uchungu
unatofautina kwa kila mama na mara nyingine kujifungua hakutabiriki. Hii nikwa hisani ya news.un.org