Zaidi ya watu milioni saba nchini Sudan kusini sawa na theluthi mbili ya
watu wote huenda wakakabiliwa na hali mbaya ya uhakika wa chakula katika miezi
michache ijayo kusipopatikana misaada ya kibinadamu.
Onyo hilo limetolewa na shirika la mpango wa chakula duniani WFP ambalo sasa
linahaha kupata fedha za kutosha kutoa msaada kwa watu hao nchini SUDANI KUSINI.
Hatahivyo mtoto Nyadane Kuony mwenye umri wa miaka minne hulia wakati anapo
hisinjaa Akiwa na babu na bibi yake waliokimbia vita huko Bentiu mwaka
2016, baba yake alifariki dunia kabla hajazaliwa na mama yake kwa sasa hayupo.
Binti huyo alianza matatizo ya utapia mlo vita vilipochachamaa nchini humo.
Hivi sasa kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula watu wamegeukia kula mianzi na
matunda mwitu. Mine Pusk Luoch ana umri wa miaka 8 tu amesema“Nimekuja
hapa kula mianzi hii kwasababu hatuna chakula.”
Maelfu ya wakimbizi wa Sudan kusini
wanaendelea kumiminika katika nchi jirani ikiwemo Kenya ambako kambi ya Kakuma
inahifadhi zaidi wakimbizi 106,000 kutoka sudan kusini. WFP inawapa msaada wa
chakula wanapo pokelewa tu kama anavyofafanua Martin Karimi msemaji wa shirika
hilo nchini Kenya.
“Tunapokea takribani watu elfu moja kila
mwezi, wanapowasili WFP inawapa mlo wa moto kabla hawajapewa vipande vya ardhi
ambako wataendelea kupokea mgao wa chakula pamoja na fedha taslim kutoka WFP.”Hivi
sasa WFP inatoa chondechonde kwa wahisani na wafadhili kutoa fedha ili kusaidia
shirika hilo kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi hao. Tembelea www.news.un.org
Sudani Kusini njaa yapoteza matumaini kwa wana nchi ambapo watoto ndio wanao teseka zaidi kukabiliana na jangahilo.
Leave a comment