Watoto wa Syria hawana haki kama wengine?
Picha: UM/Jean-Marc Ferré
Watoto Syria wakisimama katika hema katika makazi yao kwenye kambi ya
wakimbizi wa ndani, Baraza la haki za
binadamu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao mahsusi kuhusu ukiukwaji wa
haki za binadamu hususan watoto nchini Syria.
Akihutubia kikao hicho mjini Geneva, Uswisi, mratibu wa Umoja wa Mataifa
kuhusu masuala ya kibinadamu nchini Syria Panos Moumtzis amesema kutwa kucha
watoto wa Syria hususan eneo la Ghouta Mashariki sasa wanakabiliwa na mmiminiko
wa makombora.
Amesema baada ya miaka mitano ya kuishi kwenye eneo lililozingirwa, sasa
wanaishi kwenye mahandaki yaliyojaa kupindukia bila kufahamu kesho yao itakuwa
vipi.Tembelea https://news.un.org/swa.