Wakati Umoja wa Mataifa na wadau wake wanapambana kukomesha ukatili
na unyanyasaji dhidi ya wanawake, serikali ya Tanzania nayo pia ipo mstari wa
mbele kuhakikisha hakuna mwanamke au mtoto wa kike atakayebaki nyuma
katika mpango huo madhubuti.
Akizungumza na Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa punde tu baada ya
kuhutubia mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake jijini New York,
Marekani,
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, Watoto na Wazee nchini Tanzania Sihaba Nkinga
amesema..Kuhusu tathmini na ufuatiliaji wa mpango huo ulioanzishwa mwaka 2011
ukijikita na ukomeshaji wa ukatili dhidi ya wanawake chini ya ofisi ya Waziri
Mkuu, Bi Nkinga amesema serikali iliamua kutengeneza mpango zikijumuishwa
secta zisizo za kiserikali kupinga ukatili huo unapo mkatili mama mtoto alieko
tumboni nae ana athilika. Taarifa hii nikwa mjibu wa UN RADIO