Shirika la Umoja wa Mataifa
la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR, limeshtushwa na ongezeko la idadi ya
wakimbizi wa Cameroon wanaosaka hifadhi Nigeria ambapo idadi
yao sasa imefikia 20,000.
Aikaterini Kitidi ambaye ni
msemaji wa UNHCR, mjini Geneva, Uswisi amesema hayo akizungumza na
waandishi wa habari kuwa taarifa kutoka kwa washirika wao ni
kwamba zaidia ya asilimia 95 ya wasaka hifadhi wanakosa huduma muhimu kama
chakula na malazi.
Amesema baadhi ya familia wamebakiza mlo mmoja kwa siku moja
kutokana na upungufu wa chakula.
“Hadi sasa
ofisi yetu imekuwa ikifanya kazi ya kutoa huduma kwa
wakimbizi hawa chini ya mpango wa dharura wa dola 18 milioni. Hata hivyo,
hadi sasa hakuna fedha zilizopokelewa, na kusababisha changamoto kubwa na
mapungufu katika utoaji huduma.”
Na kuhusu ushirikiano baina ya UNHCR na serikali ya Nigeria Bi Kitidi amesema
“Mapema mwezi huu, mamlaka nchini Nigeria ilitenga ardhi kwa
UNHCR ambayo inapaswa kuruhusu makazi ya wakimbizi hao ili kuhakikisha usalama
wao. UNHCR inaendelea kushirikiana mamlaka husika kususu kuhamishia makazi
ya wakimbizi angalau kilomita 50 kutoka mpakani, kulingana na sheria za
kibinadamu.” Hii nikwamjibu wa UNRADIO