Usalama na afya ya watoto wakimbizi wa Rohingya zaidi ya laki tano wanaoishi
katika kambi zilizo na msongamano mkubwa na makazi yasiyo rasmi nchini
Bangladesh iko hatarini hayo yamesemwa na shirika la Umoja wa Mataifa la
kuhudumia watoto UNICEF.
Onyo hilo la UNICEF limekuja wakati msimu wa vimbunga na mvua za Monsoon ukijongea
nchini Bangladesh , likisema kwamba hali ya kibinadamu ambayo tayari ni mbaya
kwa watoto zaidi ya 520,000 sasa huenda ikawa zahma kubwa ambapo maelfu ya
watoto watakabiliwa na hatari ya magonjwa, mafuriko, maporomoko ya udongo na
pia watoto kutawanywa zaidi.
Kwa mujibu wa Edouard Beigbeder mwakilishi wa UNICEF Bangladesh amesema
maji yasiyo salama , upungufu wa vifaa vya usafi na mazingira machafu
vinaweza kusababisha mlipuko wa kipindupindu na homa ya ini aina ya E, magonjwa
ambayo hukatili haraka maisha ya kina mama wajawazito na watoto. Christopher
Boulierac ni msemaji wa UNICEF.
Amesema kuwa msimu huo wa
monsoon pia utaweka hatarini makazi ya wakimbizi, mfumo mzima wa maji, vyoo na
miundombinu mingine ambayo inasaidia wakimbizi wa Rohingya zaidi ya 650,000
walioingia Bangladesh tangu Agosti 2017 Taarifa hii nikwa mjibu wa UN RADIO.
Watoto zaidi ya 520,000 sasa huenda ikawa zahma kubwa ambapo maelfu ya watoto watakabiliwa na hatari ya magonjwa,na mafuriko.
Leave a comment