Tangu mwezi disemba mwaka 2013,
Sudan K usini imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Maelfu ya watu
wamekimbilia nchi jirani na wengine wamesaka hifadhi kwenye maeneo mengine ya
nchi. Hata hivyo hivi sasa wengine wameamua kurejea na kilio chao sasa ni kwa
mwenyezi Mungu.
Nchini Sudan Kusini msimu wa mvua
ukitarajiwa kuanza, baadhi ya wakimbizi wa ndani na hata wale waliokimbilia
nchi za jirani wameamua kurudi nyumbani angalau kuendelea na maisha yao.
Hapa ni Kajo Keji, mji ulioko jimbo la Equitoria ya Kati nchini Sudan
Kusini. Eneo hilo lilikuwa mahame tangu kuanza kwa mzozo nchini humo mwezi
disemba mwaka 2013.Hivi sasa nuru ya amani imewezesha baadhi ya wakimbizi
kurejea ili kuendeleza maisha yao na miongoni mwao ni Grace Kobong akikagua lililokuwa shamba lake la mihogo hatahivyo
amesema.
“Napanga kurejea hapa na kuishi. Mwanangu alifariki dunia na sina mtu wa
kunisaidia. Alizoea kuja na kunisaidia kuvuna mihogo lakini sasa hayupo.
Nimerejea ili nilime na nasaka mbegu za mahindi nipande.” Kwa
taarifa zaidi tembelea https://news.un.org/sw/