Katika jamii zetu za kitanzania suala la michezo kwa watoto wadogo ambao hawajaanza shule, limekuwa likichukuliwa kiholela
sana. Lakini kisaikolojia michezo ni muhimu sana kwa watoto wadogo
ambao hawajaanza au ambao wameanza shule tayari. Michezo ni muhimu sana
kwa watoto wagogo kwa sababu humsaidia mtoto kukua katika nyanja mbali
mbali zikiwemo
kiakili, kimwili, kihisia na kijamii pia.
Katika makala hii fupi sitaangazia sana kwa kina swala la michezo kwa
watoto wetu wadogo ila nitatoa dondoo za muhimu chache ili kuwasaidia
wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ili waweze kuweka kipaumbele katika
michezo kwa watoto wao wadogo ili kuleta tija katika maendeleo ya watoto
wao walioanza elimu ya awali au wale ambao hawajaanza elimu ya awali
ili waweze kuendelea katika nyanja mbali mbali kama nilivyokwisha
ainisha hapo awali.
Michezo ni muhimu sana hasa kwa watoto ambao
bado hawajaanza shule za awali (chekechea). wazazi wengi wa kitanzania
hupuuzia sana swala la michezo kwa watoto wao wadogo, na kulifanya kuwa
jukumu la watoto wenyewe “michezo haisababishi mtoto asijifunze bali
humsaidia mtoto kujifunza”
ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO WAZAZI NA WALEZI WANAWEZA KUZITUMIA ILI KUHAKIKISHA MICHEZO KWA WATOTO WAO
1) Wazazi au walezi wawape watoto vitu mbalimbali vya kuchezea mfano, modoli, mipira ya miguu, karatasi n.k
2) Wazazi wa wasisitize watoto wao wacheze michezo mbali mbali mfano,
kukimbia, kuruka, kuimba, kuhesabu, kujenga, kutengeneza maumboi
mbalimbali n.k
3) Wazazi au walezi watenge muda wa kucheza na watoto wao, pia waulize maswali kuhusu michezo wanayo icheza mara kwa mara
4)Wazazi wawaangalie watoto wao wakati wanacheza ili wasiumizane
ZIFUATAZO NI FAIDA ZA MICHEZO KWA WATOTO
1) Huwasaidia watoto kukua kiakili, michezo huwafanya watoto wawe na akili nyepesi katka kujifunza
2) Huwasaidia watoto kukuza lugha, wanapata misamiati mipya wakiwa na watoto wenzao
3) Michezo pia huwasaidia watoto kuimarika misuli na kukua kimwili, hii
ni kwa michezo inayohusisha mazoezi ya viungo mfano, kucheza mpira,
kukimbia n.k
4) Huwasaidia watoto kukua kijamii, mfano kuhusiana wao kwa wao
5) michezo pia huwaandaa watoto tayari kwa kuanza shule, huwasaidia kujiamini pia wanapoingia shuleni
ZIFUATAZO NI HASARA ZA KUKOSA MICHEZO YA KUTOSHA KWA WATOTO
Watoto wakikosa michezo kwa kiwango kinachowapasa wanaweza kupata madhara yafuatayo
a) wanakuwa wazubaifu sana, ukiona mwanao ni mzubaifu sana ujue hajapata michezo vizuri
b) watoto pia wanakuwa wagumu kuelewa
c) kadhalika watoto wanapokosa michezo vizuri wanashndwa kujiamini hata wanapoenda kuanza shule
MWISHO
Nakushauri, mzazi au mlezi kubadilisha sasa, mtazamo uliokuwa nao
kuhusu michezo, na naamini sasa utamruhusu na kumsimamia mwanao pia
kumwezesha katika michezo yake ili kumwandaa apate malezi na ukuaji
jumla kwa maendeleo yake na Tanzania mpya ya kesho. asanteni sana.