Mbali ya mila na desturi, mazingira na mazoea vimetajwa kuwa chachu
ya kumkosesha elimu mtoto wa jamii za wafugaji nchini Tanzania kama Wamaasai na
Wamang’ati.
Ingawa elimu inatajwa kuwa ni ufunguo wa maisha , lakini sio kwa wote nchini
Tanzania na hususani katika jamii za wafugaji hasa wa Kimaasai na Kimang’ati,
ambako kwa miaka nenda miaka rudi jamii hizo zimejikita ktika ufugaji na
hasa wa kuhamahama hali inayofanya kuwa vigumu watoto wengi kwenda shule ,
lakini kwa watotowakike changamotoni kubwa zaidi kwani mila zinamuuona kama
asiye na thamani, lakinipia nafasi yake kubwa ipo katika malezi ya familia na
jikoni.
Juhudi kubwa zinaendelea kufanyika nchini humo na serikali, wanaharakati na
hata mashirika ya Umoja wa Mataila likiwemo la kuhudumia watoto UNICEF
kuhakikisha haki ya elimu kwa jamii hizo inatambulika lakini bado kuna
changamoto kubwa.
John Kabambala kutoka Radio washirika Tanzania Kidstime amezitembelea baadhi
jamii hizo mkoani Pwani ili kupata maoani ya vijana kuhusu elimu. Akianza na
Moi Loita kutoka katika jamii ya Kimasaai aliyebahatika kupata elimu.