Naye
Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Henrietta H. Fore amesema maziwa ya mama ni
muhimu kwa afya ya muda mrefu ya mtoto na hupunguza gharama za matibabu
ya afya kwani huepusha magonjwa kama vile kuhara.
Hata hivyo viongozi hao wamesema uamuzi wa mama kumnyonyesha mtoto
wake kwa miaka miwili mfululizo unahitaji ushirikiano kutoka ngazi ya
familia hadi kitaifa.
Hatua hizo 10 ni pamoja na hospitali kuweka sera ya unyonyeshaji na
kuzingatia kanuni za kimataifa za kuwapatia watoto wachanga maziwa ya
kopo iwapo inalazimika kufanya hivyo, na será hizo ziwe bayana kwa
wahudumu wa afya.
Halikadhalika hospitali zijadiliane na wajawazito na familia zao
kuhusu umuhimu wa kunyonyesha mtoto na pia watoto wachanga wasipatiwe
kitu kingine chochote zaidi ya maziwa ya mama labda tu ikiwa kuna tatizo
la kitabibu.
Mwongozo pia unataka mama aelekezwe athari za matumizi ya kutumia
chupa za kunyweshea mtoto maji au maziwa na hata mpira wa kumwekea mtoto
mdomoni ili asilie.Taarifa zaidi UN Radio.