Mtoto anaponyonyeshwa miaka miwili mfululizo bila kupatiwa kimiminika
chochote ataepusha gharama kubwa zinazotumika kutibu magonjwa kama vile kuhara,
magonjwa ambayo husabaisha na matumizi ya maji yasiyo safi na salama katika
kumwandalia maziwa mbadadala badala ya yale ya mama.
Hospitali si tu sehemu ya matibabu bali pia ni pahala ambapo panatakiwa
kujenga msingi wa afya bora na hivyo kuokoa vifo, amesema Mkurugenzi Mkuu wa
shirika la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus kufuatia uzinduzi wa mwongozo mpya wa
shirika hilo na lile la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuimarisha unyonyeshaji wa
watoto.
Mwongozo huo una hatua 10 zinazolenga ngazi ya kisera hospitali na pia
huduma yenyewe ya unyonyeshaji ambapo mashirika hayo yanasema ukizingatiwa
utaokoa maisha ya watoto 820,000 kila mwaka wenye umri wa chini ya miaka 5.
Dkt. Tedros amesema katika hospitali nyingi au jamii yoyote ile iwapo mtoto
anaweza kunyonyeshwa maziwa ya mama yake au la kunaweza kuleta tofauti kubwa
kati ya kifo na uhai. Hii taarifa nikwamjibu wa UN RADIO.