za utotoni ni changamoto kubwa nchini Tanzania na hususani katika
maeneo ya vijijini. Serikali ya nchi hiyo ikishirikiana na wadau
mbalimbali wa elimu, ustawi wa jamii na mashirika ya kitaifa na
kimataifa kama la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF
wanaelimisha jamii wakiwemo wasichana wadogo mashuleni athari za mimba
hizo.
Pelosi
alikuwa na ndoto za kuwa mhadisi au daktari siku moja lakini sasa ndoto
zake zimeishia kulea mtoto baada ya kupata ujauzito akiwa kidato cha
pili kwenye shule ya sekondari ya Dumila mkoani Morogoro nchini
Tanzania.
Akijutia kilichomsibu anaeleza sababu za tupa jalalani ndoto zake
Na je baba wa Pelosi alialichukua hatua gani baada ya tarifa hizo za masikitiko?
Pelosi ni kama tone la maji baharini ukilinganisha na idadi ya wasichana wanaokatiza masomo kutokana na mimba za utotoni.
Kwa mujibu wa takwimu za afisa elimu na Mganga mkuu mkoa humo Frank Jacob, amesema waathirika
wakubwa ni wanafunzi wa shule za msingi kati ya umri wa miaka 13-15 ,
lakini wengi zaidi ni wa sekondari kati ya miaka 16-18 ambapo kuanzia
Julai hadi Septemba 2017 watoto 301 walikatiza masomo kutokana na mimba
za utotoni na hatua madhubuti zisipochukuliwa basi kutakuwa na mtihani
mgumu wa kutimiza lengo la maendeleo endelevu nambari 4 la elimu bora
likijuisha wasichana na wavulana ifikapo 2030.