Hii ni awamu ya pili ya watoto kuachiliwa huru katika mpango unaodhaminiwa
na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa mataifa la UNICEF.Kufuatia hatua
hiyo, mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan Kusini, Mahimbo Mdoe, amesema hakuna
mtoto anayepaswa kubeba bunduki na kupigana.
Amesema kila mtoto anayeachiliwa huru, siku hiyo huwa ndio mwanzo wa
maisha yake mapya na kukariri kuwa UNICEF inajivunia kuwasaidia
watoto hao warejee katika familia zao na kuanza maisha mapya.Wakati wa sherehe
ya kuachiliwa rasmi,mjini Yambiyo watoto hao walipokonywa silaha na kupatiwa
nguo za kiraia na baadaye watapatiwa ushauri nasaha kama sehemu ya kuwajumuisha
katika maisha mapya, mpango ambao unatekelezwa na UNICEF.
Miongoni mwa watoto hao waliochiliwa huru, 112 ni wavulana ilhali wasichana
ni 95.Wote walitoka katika makundi mawili ya Sudan National Liberation
Movement, -SSNLM- ambalo lilisaini mktaba wa mani na serikali mwaka 2016 pamoja
na lile la Sudan People’s Liberation Army-upande wa upinzani, SPLA-IO.UNICEF
inasema watoto wengine takriban 1,000 wataachiliwa huru miezi michache
ijayo. Taarifa nikwa mjibu wa radio ya umoja wa mataifa UN Radio.