Ili
kutimiza ajenda ya kimataifa ya maendeleo yaani SDG’s hapo mwaka 2030 hususani
kwa mataifa ya Afrika, basi ni lazima kuhakikisha afya kwa wote inapatikana. Hayo yamesemwa na Profesa Francis
Omaswa mkurugenzi mtendaji wa kituo cha afya cha Afrika kwa ajili ya afya ya
kimataifa na mabadiliko ya kijamii nchini Uganda, alieyehudhuria mkutano
wa Dunia wa kikanda wa afya uliofanyika mjini Coimbra , Ureno.
Akizungumza na UN News kandoni mwa mkutano huo Profesa Omaswa amesema
kikubwa walichojikita nacho kikubwa , Bi Monica Ferro mkurugenzi wa shirika la
Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA katika ofisi ya
Geneva Uswisi amesema amewakilisha shirika lake kwenye mkutando huo ili
kujadili umuhimu wa kuwekeza katika afya ya mwanamke
Ni muhimu kuwekeza katika afya yao, ni muhimu
kuwekeza katika upatikanaji wa uzazi wa mpango ili kuwapa fursa ya kupanga
mwelekeo wa maisha ya baadaye katika kupata elimu ya
kutosha ili kuwapa uwezo na ujasiri wa kuamua
maisha yao ya baadaye na pia fursa ya ajira nzuri kama ilivyo kwenye
mpango wetu wa kutomuacha mtu yeyote nyuma.
Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la afya duniani WHO, uliokunja jamvi tarehe
20April mwaka huu na uliwaleta pamoja washiriki zaidi ya 100, mashirika mbalimbali
ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na wataalamu kutoka Amerika, Ulaya, Asia ,
Amerika Kusini na Afrika ambayo imewakilishwa na takribani washiriki 100, ili
kukuna vichwa na kutoka na mbinu za kuhakikisha lengo la afya kwa wote duniani
linatimia. Taarifa hii ni kwa mjibu wa UN Radio.
Who Afrika yasema afya kwa wote nilazima ipatikane ifikapo mwaka 2030.
Leave a comment