Ripoti ya hivi karibuni ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
watoto duniani UNICEF, imebaini kuwa licha ya vita vya zaidi
ya miaka 7 nchini Syria, watoto milioni 4.9 wameendelea kupata elimu, japo
katika mazingira magumu .
Geert Cappelaere. ambaye ni mkurugenzi wa UNICEF ukanda wa Mashariki
ya kati na kaskazini mwa Afrika amesema, misaada kutoka kwa wahisani na
kazi nzuri ya kujitolea inayofanywa na waalimu nchini humo ndio sababu
kuu ya kufikia mafanikio hayo ya elimu kwa watoto.
Aidha ripoti imesema zaidi ya asilimia 90 ya watoto ambao wanapata
elimu katika shule za umma wapo Syria na wengine ni wakimbizi wa Syria
walioko Lebanon na Jordan ambao wanaendelea kupata elimu katika shule za
umma za nchi hizo.
Kwa mujibu wa UNICEF japo wamefanikiwa kwa kiasi, mgogoro wa Syria
ambao umedumu kwa zaidi ya miaka saba umewakosesha elimu zaidi
ya watoto milioni 2.8, ambapo tangu mwaka 2011 shule Zaidi ya
309 zimeharibiwa.
Ripoti imeongeza kuwa shule moja kati ya
3 zimesambaratishwa kabisa na kusababisha zaidi ya asilimia 40 ya
watoto wenye umri kati ya miaka 15 na 17 kutokuwa shuleni na
kuishia kwenyemakundi ya kigaidi baada ya kurubuniwa na wahalifu. Taarifa
hii ni kwamjibu wa Radio washirika UN
Radio kutoka New York.