Wanafunzi 56,000 kutoka shule
100 za eneo la Karamoja, kaskazini-mashariki mwa Uganda sasa hawatokuwa na hofu
tena ya magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji safi na salama kufuatia
makubaliano ya Umoja wa Mataifa na Korea Kusini.

Makubaliano
hayo yanahusisha mradi wa miaka mitano ya kujenga miradi ya maji safi na salama
na huduma za kujisafi katika shule zilizoko wilaya zote 10 za Karamoja.

Shirika
la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF ambalo ndilo limetia saini
makubaliano hayo na Korea Kusini limesema kupitia mradi huo watajenga vyoo,
mitambo ya nishati ya jua pamoja na kuweka maji safi na salama kwa ajili ya
kunywa na kujisafi ikiwemo kunawa mikono. Wanafunzi wa kike pia watapata elimu
kuhusu hedhi salama.

Mwakilishi
wa UNICEF nchini Uganda Doreen Mulenga, amesema mradi utasaidia wanafunzi
kuepuka utoro, magonjwa ya kuambukiza yatapungua na watoto watakuwa na fursa ya
kujifunza kwa kina zaidi na hivyo kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu.

Mathalani
amesema maji ya kunywa yatapatikana ndani ya umbali wa mita 500 shuleni badala
ya wanafunzi kulazimika kutembea kwa nusu saa kusaka maji hayo kama wafanyavyo
hivi sasa.

Mradi
huo unagharimu dola milioni 10 ambapo Korea Kusini inachangia dola milioni 8 na
UNICEF dola milioni 2. Taarifa hii nikwa mjibu wa UN Radio.