Watoto wakimbizi nchini Rwanda sasa wanaona nuru katika maisha yao
kutokana na ushirikiano kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
wakimbizi UNHCR na mfuko wa H&M.
Ubia huo unawezesha watoto wakimbizi nchini Rwanda kupata elimu kwa kuwa
wanaishi katika makazi salama na zaidi ya yote wanapatiwa vifaa vya shule na
kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye.Miongoni mwa wanufaika wa ushirika huo
ni mwanafunzi Godfried kutoka Burundi ambaye sasa anaishi kwenye kambi ya
wakimbizi ya Mahama nchini Rwanda.
Godfried anasema tangu akiwa mtoto mdogo alikuwa na ndoto ya kuwa mwandishi
wa habari, lakini machafuko nchini Burundi yalififisha ndoto hiyo.Alilazimika
kukimbilia Rwanda ambako sasa angalau nuru inamuangazia.Sasa yuko
salama kambini na ndoto ya Godfried ya kuwa mwandishi wa habari inaonekana
kutimia kwa kuwa..
“Sasa niko salama na
ninahudhuria darasani. Nina furaha kwamba wanatupatia vifaa vya
shule .”UNHCR inasema duniani kote ni asilimia 61 tu ya watoto
wakimbizi ndio wana fursa ya kuendelea na masomo ukimbizini. Kwa taarifa zaidi
tembele UN RADIO.