Ripoti hiyo imesema kuwa ukame uliosababishwa na ukosefu wa
mvua,mfumuko wa bei na migogoro ya kivita katika baadhi ya nchi za Afrika
magharibi kama Mauritania, Kaskazini mwa Senegal, Mali, Niger Burkina Faso na
Chad mwaka jana vimesababisha ukosefu mkubwa wa chakula .
Mashirika hayo likiwemo la chakula na kilimo duniani FAO , la
watoto UNICEF na mpango wa chakula duniani WFP yamesema kupitia ripoti
hiyo kwamba msaada unahitajika haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya
mamilioni ya raia katika ukanda huo.
Abdou Dieng ambaye ni Mkurugenzi wa WFP kanda ya Afrika magharibi na
kati amesema wamepata taarifa kuwa, kutokana na janga hilo la njaa, baadhi ya
raia wamepunguza milo yao kwa siku huku wanafunzi wakitoroka shule
kutokana na ukosefu wa chakula
UNICEF, FAO NA WFP, waliunda kikosi kazi ili kuweza kukabiliana na matatizo
ya dharura yanayowakabili raia katika nchi zilizoko ukanda wa Sahala, huku
wakikaribisha misaada mbalimbali kutoka kwa wahisani ili waweze kusaidia
mipango ya muda mrefu.
Kupitia ripoti hiyo kila shirika limetaja kiwango cha fedha inachohitaji kwa
operesheni zake ambapo WFP inahitaji dola milioni 284 ,
UNICEF dola milioni 264 na FAO dola milioni 128 ili kuweza kuwafikia
wahitaji laki 9 katika nchi hizo za Afrika maghribi. Taarifa hii nikwa
mjibu wa radio ya umoja wa mataifa UN RADIO.