Mtoto mmoja raia wa Syria ambaye amekuwa akikimbia vita kwa miaka mitano
sasa bado hajaweza kupata unafuu kwa kuwa kila aendako ikiwemo nchini Libya
bado hali ni ngumu.
Ni mtoto Bassam mwenye umri wa miaka minane akisema kuwa hawezi kurejea
Misrata kwa kuwa kuna vita. Anasema angetaka warejee nchini mwao Syria.Bassam
na familia yake akiwemo baba, mama na nduguze walikuwa Misri kwa matibabu
wakati vita vinaanza nchini Syria.
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF,
familia hii ilihamia Libya kusaka maisha ambako nako hali si shwari.Kila mara
milio ya risasi bila kusahau vitendo vya kikatili kutoka kwa makundi
yaliyojihami.Baba mzazi wa Bassam, Ali Muhammed anasimulia ukatili alioshuhudia
mwanae.
“Walifunga mwili wa mwanadamu
nyuma ya gari na kuuvuta kupitia barabara kuu na Assam aliona hiyo. Kwa
sasa kila mara huamka kutoka usingizini akiwa na uoga.”
Vita na umaskini vimemuathiri mtoto huyo na sasa amekondeana akiwa na uzito
wa chini ya kilo 20 huku mwenyewe akikumbuka uzito wake wa awali.Bwana Muhammed
anataka wahamie Ulaya akiamini kuwa huko maisha ni bora kuliko Libya hata hivyo
wanahofia kuvuka baharí ikizingatiwa taarifa nyingi zinazoonyesha watu wakifa
majini. Taarifa hii nikwamjibu wa radio ya umoja wa mataifa.
vita nihatari kwa taifa.
Leave a comment