Elimu yasalia ndoto kwa watoto wengi
duniani hususan wa kike, sasa vijana wenzao wamechukua hatua madhubuti.Umoja wa
Mataifa limepokea ombi lililotiwa saini na vijana milioni 1.5 duniani la kutaka
uwekezaji zaidi kwenye elimu.

Ombi hilo limewasilishwa jijini New
York, Marekani na vijana watatu kwa Katibu Mkuu Antonio Guterres na mjumbe
maalum wa elimu Gordon Brown.Hatua ya vijana hao kutoka Kenya Sierra Leone na
India inazingatia kuwa hivi sasa , watoto na barubaru milioni 264 hawako
shuleni, fursa ya kupata elimu kuanzia ile ya chekechea hadi elimu ya juu
ikizidi kuwa finyu.

Bwana Guterres amesema hali ni mbaya
zaidi kwa watoto wa kike na wasichana ambao wao wanalazimika kusalia nyumbani
kufanya kazi za kuteka maji na kulea familia ilhali kaka zao wanakwenda shule.Watoto
huko Sudan Kusini, katikati ya mzozo, wakisaka elimu kwa udi na uvumba.

Amesema huko ni kuwakosesha haki yao
ikiwemo ya kuendeleza vipaji vyao na kustawi ili hatimaye waweze kuchangia
katika maendeleo yao na jamii zao.

“Ndoto yetu ya mustakhbali endelevu inategemea
kusaidia watoto wote wapate haki yao ya elimu. Hii inaamanisha mambo matatu;
waanze mapema, kupatia kipaumbele walio pembezoni na kuchagiza usawa. Katika
dunia yetu inayobadilika kwa kasi kubwa hatuwezi kukubali watoto milioni 250
washindwe kupata stadi za msingi.”

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu
amesema…
amesema…
“Ndio maana mapendekezo
haya ya chombo cha kimataifa cha uwekezaji kwenye elimu yanaweza kuwa muhimu.
Hebu na tufanya yasiyowezekana yawezekane.”

Tukio hilo lilishuhudiwa pia na rais
mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye ni kamishna wa jopo la watu mashuhuri
la Umoja wa Mataifa kuhusu elimu.Punde baada ya uzinduzi, jopo hilo
lilizungumza na waandishi wa habari ambapo Kikwete aliulizwa ni kwa jinsi gani
chombo hicho kilichozinduliwa kitaweza kusaidia Tanzania.

“Tatizo limekuwa ni kiwango,
iwe ni cha walimu au vifaa vya kama vile vitabu na vifaa vingine . Serikali
imeongeza bajeti ya elimu, imekuwa ni kipaumbele kwa zaidi ya asilimia 20.
Lakini hiyo pekee haikutosheleza ndio maana serikali inahitaji msaada wa jamii
ya kimataifa na ndio maana tunaona hatua kama hii ya chombo cha kimataifa cha
kuchangisha fedha kwa ajili ya elimu kitakuwa na faida kubwa kwa serikali ya
Tanzania.”