Hali ya kuwa tegemezi wa misaada inadumaza nchi nyingi kiuchumi na hata
kijamii, ikiwemo katika maendeleo ya elimu. Sasa nchi masikini na zenye kipato
cha wastani zinachagizwa kuondokana na hali hiyo ili kujikwamua na mzunguko wa
umasikini ikiwemo elimu duni na jopo la kimataifa la ufadhili kwa ajili ya
elimu limezindua ombi la dola bilioni moja kuzisaidia nchi hizo kuepukana na
utegemezi.
Changamoto kubwa za elimu zinapatikana katika nchi zenye kipato cha chini na
cha wastani na ni kutokana na kuwa tegemezi wa misaada ya wahisani kwa masuala
mbalimbali ikiwemo suala la elimu sasa jopo la kamisheni ya ufadhili wa elimu
imezindua ombo la dola bilioni moja kuzisaidia nchi hizo. Selina Jerobon na
tarifa kamili,Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa wajumbe wa jopo la kimataifa la
kamisheni ya ufadhili kwa ajili ya elimu Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa jijini New York
Marekani Rais huyo msataafu wa Tanzania amesema mkakati wa jopo hilo la
ufadhili wa elimu ni kuhakikisha nchi nyingi hususani barani Afrika zinatoka
katika kipato cha chini cha kutegemea misaada ikiwemo ya elimu na kuingia
katika kipato cha wastani jambo ambalo litainua uchumi wa nchi hizo na itakuwa
chachu ya kukuza pia kiwango cha elimu hata zikifikiwa kiwango hicho
haimaninishi ndio zimeshinda kabisa mtihani. Taarifa hii nikwamjibu wa UN
Radio.