yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Dr.
Tedross Adhamo Ghebreyesus wakati akifungua baraza kuu la 70 la afya
dunia hii leo mjini Geneva Uswisi, na kuongeza kwamba, “hakuna bidhaa
yoyote iliyo na thamani zaidi afya, ni taasisi iliyo na jukumu la
kuteteta afya ya watu bilioni 7, hivyo inabeba jukumu kubwa na ni
lazima iwe katika kiwango cha juu.”
Amesema na kumbusho kubwa la wajibu huo ni pale panapojitokeza
milipuko ya magonjwa na kudhihirisha umuhimu wa watu ambao WHO
inawahudumia.
Amesema amefurahishwa na ari na kujitoa kwa wahudumu wa afya wa
shirika hilo ambao kila uchao wanaweka maisha yao hatarini ili kuokoa ya
wengine. La msingi ni kujiandaa akitolea mfano mlipuko wa Ebola
unaoendelea hivi sasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC
akisema ingawa mlipuko umeingia mjini lakini maandalizi ya kuukabili ni
mazuri kuliko ilivyokuwa 2014.
Naye Dkt. Peter Salama, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WHO masuala ya
dharura WHO akifafanua kuhusu kuanza leo kwa chanjo ya mzunguko ya Ebola
ambayo bado iko kwenye majaribio, iitwayo Zaire Ebola virus na
ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa huko Guinea amesema, “Inaitwa
chanjo kwa mfumo wa mzunguko kwa sababu hii si kampeni ya kawaida ya
chanjo ambayo unapatia chanjo wakazi wote wa eneo fulani.
Hii ina
walengwa.Kimsingi unabaini mgonjwa, halafu unabaini watu wote waliokuwa
karibu na mgonjwa huyo, na wengine waliokuwa karibu na hao, wakiwemo
wahudumu wa afya na hiyo inakupatia mzunguko uliomzigira mgonjwa.”
Na kwa mantiki hiyo Dkt. Ghebreyesus amehimiza “Ni
lazima tuchukue hatua za haraka kwa kila tunalolifanya , kwa sababu
kila wakati tunaoupoteza ni suala la baina ya uhai au kifo.” Ndio
maana WHO inashirikiana na wadau kukomesha kifua kikuu au TB, imeanzisha
miradi mipya kutokomeza malaria, imezindua mikakati ya kutokomeza
utipwatiwa na mikakati mingine mingi kuhakikisha malengo ya afya
yanatimia ifikapo 2030.
Kwa mantiki hiyo WHO imeharakisha kuanzisha mkakati wa 13 wa kazi
zake ujulikanao kama GPW, lengo likiwa kuchagiza afya bora, kuifanya
dunia kuwa salama na kuhudumia wasiojiweza kwani, “hatutoikubali
dunia ambayo watu wanaugua kwa sababu ya hewa wanayovuta haifai kwa
maisha ya binadamu, hatutoikubali dunia ambayo watu wanapaswa kuchagua
baina ya ugonjwa na umasikini kwa sbabu gharama za kulipia huduma kutoka
mifukoni mwao.”
Na ili hili lifanikiwe amesema kuna masula matatu ya kuzingatia, mosi ni kuwa
na shirika la WHO lililo imara na linaloleta mabadiliko, pili kuwa na
mkakati wa kuleta mabadiliko kulifanya shirika hilo kufanya kazi vizuri
na kuzaa matunda na tatu lakini pia kuhakikisha suala la jinsia linapewa
uzito mkubwa.
Baraza hilo kuu la afya duniani limewaleta pamoja nchi wanachama,
wataalamu , wadau wa afya na wanaharakati kutoka kote duniani na
litakunja jamvi tareje 26 mwezi huu wa Mei. Taarifa hii nikwamjibu wa Radio ya Umoja wa mataifa UN RADIO.