Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vita na janga la kibinadamu nchini humo vimesababisha watoto kulazimika kufanya kazi ili waweze kutunza familia zao.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vita na janga la kibinadamu nchini humo vimesababisha watoto kulazimika kufanya kazi ili waweze kutunza familia zao.
Msururu wa watoto wakiwa wamebeba magunia, makarai na magudulia yaliyojaa mchanga wakitoka fukwe za ziwa Tanganyika eneo la Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC
Watoto hao ni miongoni mwa mamia kwa maelfu ya watu ,wazee kwa watoto na wake kwa waume wanaohangaishwa na migogoro inayokumba jimbo la Tanganyika lililo mashariki mwa nchi hiyo.
Umaskini, njaa na magonjwa vinawakabili licha ya kamisaada kama vile kutoka shirika la kuwahudumia wakimbizi-UNHCR bado watoto hawa wanaendelea kupambana ili waweze kuishi.
“ Wazazi wetu hawakutufanyisha kazi kiasi hiki. Tulikuwa tunakaa tu na baba zetu wanatuletea chakula. Lakini sasa kwa sababu hatuna pa kuishi tunateseka tu.” Taarifa hii nikwamjibu WA UN radio .