Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa
UNICEF, Henrietta Fore anazuru Mali
ambako miaka sita baada ya kuanza mgogoro wa kaskazini mwa nchi hiyo ghasia
zinazidi kuongezeka huku watoto nao wazidi kunyimwa haki zao kama vile chakula,
elimu na kuishi.
Bi. Fore katika ziara hiyo ameanzia kituo cha afya cha Safo kwenye mji
mkuu wa Mali, Bamako ambapo wanawake wanapeleka watoto wao kupata huduma za
kiafya wanazohitaji.
Hii ni kwa sababu zaidi ya watoto,
850,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo,
huku wengine 274, 000 hali yao ni
taabani.
Nayo maeneo ya kaskazini na kati mwa Mali yanakabiliwa na viwango vya juu
zaidi vya utapiamlo kutokana na mapigano,sana sana karibu na eneo la Timbuktu,
huko idadi ya watoto ni zaidi ya asilimia 15.
“Watoto wa Mali kwa kweli wanateseka kimoyomoyo. Ni shida nchini Mali
kwa sababu ya kuongezeka kwa ghasia, lakini pia na umri nao
umechangia. Kwa utapiamlo watoto wengi hawakuwa wanapata chakula wanachohitaji
na tuna wasiwasi kuwa zaidi ya robo milioni ya watoto watafariki
dunia mwaka huu wakati wa mavuno madogo na hivyo ina maana kuwa kuna hofu na
hofu hiyo ni kwa watoto wote.
Hatimaye Mkurugenzi Mtendaji huyu wa UNICEF alitembea moja ya darasa la
shule ya watoto mjini Bamako.Watoto wanaonekana na ari ya masomo, ingawa
inaelezwa kuwa zaidi ya watoto milioni moja nchini Mali hawasomi na idadi yao
iliongezeka kwa asilimia 30 tangu
mwaka wa 2009 ambapo watoto 637,000 waliripotiwa kukosa masomo.
Bi Henrietta Fore akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kalabambougou,
mjini BAMAKO, MALI anatarajiwa labda kuongezea dau kutokana na jinsi
alivyoshudia hali ilivyo.
Hadi sasa shule 750 baado
zimefungwa katika sehemu za kaskazini na katikati mwa nchi hiyo kutokana na
hali za usalama ambazo zinaaathiri watoto zaidi ya 300,000 walio na umri wa kwenda shule.Wale ambao wako shuleni na
baadhi kutembelewa na mkuu wa UNICEF walifurahi na kushangilia.
“Watoto hao pia hawako shuleni, kwa hivyo
watoto zaidi milioni moja wanakosa elimu ya msingi na
wengine milioni moja hawapati elimu ya sekondari.”Hii nikwamjibu wa,
UN Radio.