Mustakhbali wa watoto Afghanistan mashakani kutokana na mapiganoTakribani
nusu ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 7 hadi 17 nchini Afghanistan hawako
shuleni.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
watoto, UNICEF iliyotolewa ikiangazia watoto wasio shuleni ikijikita zaidi
nchini Afghanistan.Sababu kuu zinatajwa ni mzozo unaoendelea nchini humo
sambamba na umaskini na ubaguzi dhidi ya watoto wa kike.
Watoto hao milioni 3.7 wasio shuleni ni kiwango cha cha juu zaidi kuwahi
kufikiwa nchini
Afghanistan tangu mwaka 2002, imesema ripoti hiyo.Asilimia 60
ya watoto hao ni watoto wa kike, hali ambayo ripoti hiyo imesema inawaweka
katika hali mbaya zaidi kwa kuzingatia ubaguzi na ukatili mwingine
wanaokabiliana nao kutokana na jinsia yao ikiwemo ndoa katika umri mdogo.
Majimbo ambamo kwayo watoto wa kike wana hali mbaya zaidi kielimu ni
Kandahar, Helmand, Wardak, Paktika, Zabul na Uruzgan.Akizungumzia ripoti hiyo,
mwakilishi wa UNICEF nchini
Afghanistan, Adele Khodr amesema kuendelea
kuchukua hatua za kawaida hakutaleta manufaa yoyote iwapo jamii ya kimataifa
inataka kuhakikisha kila mtoto anapata haki ya elimu. Hii nikwa mjibu wa UN
Radio .