Wahudumu wa mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini Uganda wakiwemo wa
Umoja wa Mataifa wanakumbana na changamoto kubwa ya kuwasaidia watoto wakimbizi
zaidi ya 250,000 waliotengana na wazazi ama walezi wao kutokana na vita na
kusaka hifadhi wakiwa peke yao nchini humo. Mwandishi wa UN nchini Uganda
John Kibego ametembelea makazi ya wakimbizi ya Imvepi Wialayani Arua
nchini humo ambako kuna asilimia kubwa ya watoto na kuandaa tarifa hii.
Wengi wa watoto hao wamekimbia vita nchini Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo, DRC, miongoni mwao ni mtoto Norman Suku Denis anayesimulia
kilichomfanya kufungasha virago
“Wakati mapigano yalipoanza, mama yangu
alimwambia baba yangu tukimbie lakini baba akasema yeye hawezi kukimbia.
Tulianza kukimbia na mama yetu lakini aliporudi nyumbani kidogo, alikuta tayari
baba yetu ameshauauwa kw akupigwa risasi. Naye mama yangu walimuua”
“Tulianza kukimbia na tukakukuta na watu amabo pia walikuwa
wakikimbia kwenda mpakani. Tulikuja nao na kukuta msichana mmoja ambaye
tulikuja naye mpaka hapa, walitupatia nyumba na hadi sasa ndiye anatulea”
Norman Suku Denis ambaye sasa ana umri wa miaka 17 na ndugu zake wadogo
wawili ni sehemu ndogo tu ya watoto zaidi ya 250,00 walio ukimbizini nchini
Uganda.Afisa wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia
wakimbizi, UNHCR, Uganda ni Duniya Aslam Khan,Anasema watoto hao wako hatarini
bila makuzi stahiki hivyo.
“Hua tunatabaini familia
ambazo zinaweza kutoa huduma ya malezi, nasi kama UNHCR na wadau wetu tunatoa
msaada kwa familia hizo. Hii ni changamoto kubwa amabyo haiwezi kushughulikiwa
na shirika moja pekee. Tunaomba wahisani kujitolea na kuwekeza zaidi katika
ulinzi wa watoto ili tuwe na kizazi salama”
Hata hivyo UNHCR Uaganda inakabiliwa na mtihani mkubwa wa ufadhili hasa
wakati huu ambapo wimbi la wakimbizi wanaomiminika nchini humo linaongezeka
kila uchao kinyume na matarajio ya shirika hilo. Taarifa hii nikwa mjibu wa radio washirika UN RADIO.