Serikali
imeweka lengo la kukusanya damu chupa zipatazo 375,203 ambayo ni ongezeko la
asilimia 60 sawa na chupa 7 kwa kila wananchi 1000 kwa mwaka 2018 pamoja na
kutenga shilingi bilioni 3 kwa ajili ya uendeshaji shughuli za
ukusanyaji wa damu salama pamoja na shilingi bilioni 10 kwa ajili ya mifuko ya
kukusanyia damu na vitendanishi.

Hayo yamesemwa leo
na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
wakati akitoa tamko la siku ya Wachangia Damu Duniani ambapo Kitaifa
yataadhimishwa jijini hapa.

“Shirika la Afya
Duniani linapendekeza kuwa, ili kukidhi mahitaji ya damu, nchi inatakiwa
kukusanya chupa 10 kwa kila wananchi 1000,’sawa na 1% ya wananchi kwa mwaka
husika”.

Aidha,Waziri
Ummy amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu Kimataifa ni “Jitoe kwa ajili ya mwingine.
Changia damu. Okoa Maisha ya mwenzio.“ (Be there for someone else.
Give blood. Share life),hivyo inaonyesha mshikamano katika uchangiaji damu,
inalenga mambo muhimu ambayo yanaonyesha thamani ya mwanadamu kama heshima,
huruma, wema na kuwajali wengine ambavyo ndio msingi wa kuendeleza uchangiaji
damu wa hiari bila malipo yoyote.

Hata hivyo amesema
bado hawafanyi vizuri katika kukusanya damu ukilinganisha na malengo “Kwa
kipindi cha mwaka 2016 tulikusanya chupa 196,735 sawa na asilimia 40 ya
mahitaji na mwaka 2017 ziliongezeka hadi kufikia 233,953 sawa na asilimia 45,” ila
kwa sasa kuna ongezeko kubwa kutokana na jitihada ya viongozi waliopo Mpango wa
Damu Salama hivi sasa”

Kwa upande mwingine
aliwahimiza Watanzania kuhusu kuchangia damu kwani ni tendo jema na la
heshima”wakati mwingine napigiwa simu watu wana mgonjwa na hakuna damu,hivyo
kila mtu aone ni wajibu wake kuchangia damu” alisisitiza Waziri Ummy Mwalimu

Amesema ongezeko hilo la upatikanaji wa damu
salama ni nguzo muhimu katika kufanikisha kupunguza vifo vya mama na mtoto,
Aidha ongezeko hili pia linaendana na uboreshaji na upatikanaji wa matibabu ya
kibingwa katika hospitali zetu za rufaa nchini kwa hivi sasa wahitaji wengi ni
wale majeruhi wa ajali hususan waendesha bodaboda ambapo imeleta ongezeko la
wahitaji wa damu

Kwa taarifa za
Mpango wa Taifa wa Damu Salama za 2017, Mikoa iliyoongoza kwenye makusanyo ya
damu ni Katavi (94% ya malengo), Lindi (79% ya malengo), Pwani (66% ya malengo).
Mikoa ambayo haikufanya vizuri ni Songwe (16% ya malengo), Mbeya (20% ya
malengo) na Tabora (22% ya malengo).

a