Dkt. Ndugulile amekutana na Waandishi wa Habari jijini Arusha kuzungumzia kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika pamoja na kufungua mafunzo ya Waandishi wa Habari za watoto yaliyoandaliwa na shirika la Plan International.
Aidha Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika kilele chake ni Juni 16, 2018 lakini yatafanyika June 13, 2018 (kesho) kwa sababu tarehe hiyo itaingiliana na ratiba ziingine.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Kitaifa yatafanyika mkoani Arusha, Kwaupande mwingine Dkt. Amezitaja haki za msingi za mtoto ziko tano zikiwemo za haki ya kuishi, kuendelezwa, kulindwa, kutobaguliwa pamoja na kushirikishwa.
Hatahivyo Ndungulile ameeleza kwamba Serikali inalinda haki na maendeleo ya mtoto ndio maana imeanzisha Idara, Sera na kutengengeneza Sheria zinazomlinda mtoto.
Pia Serikali imeboresha huduma za afya ili kuhakikisha wakina mama wanajifungulia katika vituo vya afya hivyo kuokoa vifo vya watoto, hadi sasa asilimia 97 ya watoto wanaozaliwa nchini wanapatiwa chanjo ambapo Tanzania ni nchi ya 3 kwa kuhakikisha watoto wanapata chanjo.
Pia tumeanzisha Mahakama za Watoto ambapo mashauri yanayohusiana na watoto yanasikilizwa kwa faragha pamoja na mahabusu za watoto ili kuwaweka tofauti na watu wazima.Hadi sasa tuna zaidi ya Madawati ya Kijinsia 500 nchi nzima yanayosaidia mashauri ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupatiwa ufumbuzi kwa haraka
Kwaupande mwingine Dkt. Ndungulile ametoa rai kwa wananchi kutomaliza kesi za ukatili wa watoto kifamilia badala yake kuzifikisha katika vyombo vya kisheria ili hatua za kisheria zichukuliwe kukomesha tabia hizo.
Tangu Januari hadi Disemba, 2017 jumla ya matukio 41,000 ya ukatili wa kijinsia yameripotiwa na kati ya hayo 13,457 ni ukatili dhidi ya watoto – Dkt. Ndugulile.
Matukio hayo ya ukatili wa kijinsia ni mengi kuliko matukio ya ujambazi kwa nchi nzima – Serikali imekuja na mpango mkakati wa kudhibiti ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto utakaoisha 2022 – Dkt. Ndugulile.
Kati ya mipango hiyo, Serikali imeanzisha kituo kimoja(One Stop Centre) ambacho kitajumuisha huduma za kipolisi, ushauri nasaha pamoja na huduma za kimatibabu.
Pia Dkt. Alibainisha kuwa wameanzisha namba ya simu ambayo ni 116 kwa ajili ya kutoa taarifa ya ukatili wa kijinsia ili hatua stahiki zichukuliwe .
Sambamba nahilo amekumbusha wanahabari kuwa ni kosa kisheria kusambaza picha na kumtambulisha mtoto ambaye amedhalilishwa kijinsia.
Nakuahidi kulifuatilia suala la baadhi ya wahusika wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto ya Mkoa wa Arusha ambao hawajafika katika mkutano huo.
Mwisho Dkt. Ndugulile ametoa agizo la kuanzishwa kwa tuzo za Waandishi wa Habari kuanzia mwaka 2019 ili kuwatambua waandishi wanaotoa elimu na kuripoti masuala ya ustawi na haki za watoto.
Tanzaniakidstime itaungana na watanzania kuwasaidia watoto wanaoishi mazingira Magumu.