Kuwa
mlemavu sio kulemaa na unastahili kupata haki zote kama wengine , iwe
elimu, afya na hata kutoachwa nyuma katika malengo ya maendeleo endelevu
au SDG’s, amesema seneta wa Kenya ambaye yeye mwenyewe ni mtu mwenye
ulemavu.

Wakati
nchi zikiendelea kuweka mikakati katika kuhakikisha zinafikia malengo
ya maendeleo endelevu, SDGs, bado utekelezaji wa ahadi ya Umoja wa
Mataifa ya kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma unasuasua katika
baadhi ya maeneo. Mathalani kila mtu kuwa mjuzi wa lugha yake ya taifa,
bado kuna kasoro. Je ni kwa vipi? Katika makala hii basi Grace Kaneiya
amezungumza na Dkt. Getrude Inimah Seneta katika bunge la Kenya ambaye
aliwahi kushuhudia watu walio na ulemavu wa kutosikia wakitengwa mafunzo
ya lugha ya kiswahili jambo ambalo ametaja kama unyanyapaa ambao
utakwamisha watoto hao katika siku za usoni. Dkt. Inimah ambaye ana
ulemavu wa viungo anaanza kwa kuzungumzia namna alivyopokea uteuzi
katika bunge, huu ukiwa ni muhula wake wa kwanza bungeni.