kuhusu wajibu wa kulinda maisha ya watu ni muhimu sana leo hii kuliko
wakati mwingine wowote, wakati dunia ikijitahidi kwa pamoja kuwalinda
watu hao dhidi ya mauaji ya kimbari, uhalifu wa vita, mauaji ya
kikabila na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo
akizungumza katika mjadala wa wazi wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa
mjini New York Marekani kuhusu wajibu wa kulinda maisha ya watu ,
uliopitishwa kwa kauli moja na viongozi wa dunia mwaka 2005 baada ya
kushuhudia mauaji ya kimbari ya Rwanda na Sebrenica. Lengo likiwa bayana
amesema kuongeza juhudi kwa pamoja kama jumuiya ya kimataifa kuwalinda
watu hao.
“Hata hivyo leo hii bado kuna hofu kwamba kanuni hiyo
inaweza kutumika kuchukua hatua ya pamoja kwa madhumuni mengine kuliko
yale yaliyoafikiwa katika matokeo ya mkutano wa dunia. Pia kuna wasiwasi
juu ya viwango vya pande mbili na matumizi ya kuchagua ya kanuni hizo
katika siku za nyuma.”
Na hii ndio sababu amesema uwazi katika kujadili suala hili ni
lazima, ili kuondokana na hisia zisizo sahihi na kutoaminiana
akihimiza “Tunapaswa kuunda uelewa wa pamoja na kutoa msaada mkubwa kwa
wajibu huu, kama chombo muhimu cha ulinzi na kuzuia maafa.” Taarifa hii nikwamjibu wa radio ya umoja wa mataifa UN RADIO.